KESI ya mauaji inayowakabili maofisa uhamiaji watatu wilayani Kakonko waliofikishwa kizimbani kwa tuhuma za kumuua Enos Elias itatajwa tarehe 28 Desemba mwaka huu. Anaripori Faki Sosi …(endelea).
Maofisa hao ni pamoja na Joachim Frathazaus (Kafupi), Fredrick Kyomo na Mabrouk Hatibu.
Awali watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu ya Wilaya ya Kakonko tarehe 28 Oktoba mbele ya Hakimu Kyamba ambapo Charles Mwakanyamale Mwendesha Mashtaka wa Serikali aliwasomea shtaka moja la kufanya mauaji kwa kukusudia
Watuhumiwa hao tarehe 28 Oktoba wanadaiwa walimuua kwa makusudi kijana Enos Elias (20) katika kijiji cha Chilambo.
Kesi hiyo namba 38283 ilitajwa jana tarehe 11 na kuahirishwa mpaka tarehe 28 Desemba 2023 kwa ajili ya kutajwa ambapo upande wa Jamhuri unaendelea na Mashtaka.
Leave a comment