Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Katiba Mpya, Tume Huru,Masheikh Uamsho, vyatikisa Bunge
Habari za SiasaTangulizi

Katiba Mpya, Tume Huru,Masheikh Uamsho, vyatikisa Bunge

Spread the love

MALALAMIKO kuhusu katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, muungano na masheikh wa Uamsho viliibuka bungeni wakati wa mjadala wa Hotuba ya Rais John Magufuli ya kufungua Bunge la 12, tarehe 13 Novemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mbunge wa Chonga (ACT-Wazalendo), Salum Mohamed Shafi ndiye aliyeibua hoja huku akiiomba serikali kufanyia kazi mambo hayo.

Alianza na mchakato wa Katiba Mpya ambapo aliishauri serikali kukamilisha kukamilisha mchakato.

Amesema, kwa kufanya hivyo kutasaidia kutatua changamoto zinazohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi.

Shafi alitoa ombi hilo tarehe 5 Februari 2021 bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia mjadala huo ulioongozwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson.

“Niende katika suala la mchakato wa katiba mpya, ni sehemu ambayo rais aligusia, Mheshimiwa Naibu Spika katiba hii tutakapoipata tutataua changamoto ya matatizo mbalimbali yanayo tuhusu Wazanzibar ,” alisema Shafi.

Mwanasiasa huyo alisema, katiba mpya itasaidia upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, itakayoondoa dosari za mchakato wa chaguzi nchini.

Shafi amedai kuwa, baadhi ya Watanzania hawana imani na michakato ya uchaguzi, kwa maelezo kwamba waliopewa mamlaka ya kusimamia chaguzi hizo, hawaendeshi katika misingi ya uhuru, usawa na haki.

“Leo najiuliza iweje refarii anachezesha ndani ya uwanja halafu yeye anakuwa mchezaji wa mpira na muamuzi? Kweli tutakuwa na tume huru? Tunahitaji tume huru ili tuaminishe Watanzania kwamba chaguzi hizi zinazofanywa ni huru na haki,” alisema Shafi.

Shafi alitoa mfano wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, akidai kwamba ulikuwa na dosari.

“Humu ndani sote tunafahamu namna gani wameingia humu, kila mmoja na siri yake, uchaguzi ulikuwa wa shida, ni mtihani. Leo hii ukiuliza humu, wanauliza kwani bado mimi ni mbunge?” amesema Shafi.

Hata hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), katika nyakati tofauti zilikanusha madai ya mchakato wa uchaguzi huo kutoendeshwa katika misingi ya uhuru na haki.

Katika matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na NEC na ZEC, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitangazwa kushinda kiti cha Urais wa Tanzania na Zanzibar, na kuzoa viti vya ubunge zaidi ya 360.

Wakati vyama vya upinzani Bara vikiambulia majimbo mawili – CUF moja, Chadema 1- huku ACT-Wazalendo kikiambulia majimbo mane Zanzibar.

bunge la tanzania

Akichangia hotuba hiyo ya Rais Magufuli kuhusu muungano, Shafi ameomba mamlaka husika kuhakikisha usawa unakuwepo baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Miongoni mwa mambo aliyojaidli mheshimiwa rais, ni suala zima la kudumisha muungano, muungano huu umeunganisha nchi mbili, Tanzania Bara na Zanzibar, sisi Wazanzibar, Watanzania tunahitaji wa haki,” alisema Shafi.

Shafi alisisitiza “tunahitaji muungano wa usawa na kuheshimiana.”

Akielezea changamoto za muungano, Shafi ametolea mfano katika utendaji wa mhimili wa mahakama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo amesema, kuna baadhi ya kesi zinazopaswa kusikilizwa Zanzibar, zinahamishiwa Tanzania Bara.

“Naomba ifahamike sisi Zanzibar tunayo mahakama kuu ambayo ina mamlaka ya kusikilza kesi zinazohusu masuala ya Zanzibar.

“Nilikuwa najiuliza maswali na kupata ukakasi mkubwa sana, iweje leo kesi inayopaswa kusikilizwa Zanzibar ihamishwe Bara?” amehoji Shafi.

Shafi alitolea mfano kesi ya Masheikh wa Uamsho Zanzibar ambayo inasikilizwa Tanzania Bara kwa takribani miaka nane, huku akimuomba Rais Magufuli aingilie kati suala hilo.

“Tuna kesi kadhaa, natolea mfano kesi ya uamsho hili dai liko mahakamni linaendelea, sipendi kuingilia mhimili wa mahakama lakini najiuliza sasa ni takribani miaka nane kesi hii bado iko kwenye upelelezi,” alisema Shafi.

Shafi alihoji “bado haijakamilika ushahidi wake, je hakukuwa na mamlaka Mahakama Kuu Zanzibar kusikiliza kesi hii mpaka isikilizwe Bara?

“Serikali ituambie nini shida watu hawa hadi leo wanahsikiliwa. Tunahitahji tuwatendee haki Wazanzibari,” alisema.

Mwanasiasa huyo amemwangukia Rais Magufuli, akimuomba awasamehe watuhumiwa hao kama alivyowasamehe raia wa Ethiopia zaidi ya 1,000 waliofungwa nchini kutokana na makosa mbalimbali, hivi karibuni.

“Naomba nitumie fursa hii kumuomba rais msikivu, mtetea wanyonge anayesema aombewe, nimuombe kama alivyowaachia wale Waethipopia na wale Wazanzibari na wao awaachie, awahurumie, atumie nafasi yake ya urais kuhakikisha wanatendewa haki,” amesema Shafi.

Akielezea changamoto za muungano, Shafi ametolea mfano katika utendaji wa mhimili wa mahakama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo amesema kuna baadhi ya kesi zinazopaswa kusikilizwa Zanzibar, zinahamishiwa Tanzania Bara.

“Naomba ifahamike sisi Zanzibar tunayo mahakama kuu ambayo ina mamlaka ya kusikilza kesi zinazohusu masuala ya Zanzibar. Nilikuwa najiuliza maswali na kupata ukakasi mkubwa sana, iweje leo kesi inayopaswa kusikilizwa Zanzibar ihamishwe Bara?” amehoji Shafi.

Shafi ametolea mfano kesi ya Masheikh wa Uamsho Zanzibar ambayo inasikilizwa Tanzania Bara kwa takribani miaka 8, huku akimuomba Rais Magufuli aingilie kati suala hilo.

“Tuna kesi kadhaa, natolea mfano kesi ya Uamsho, hili dai liko mahakamni linaendelea, sipendi kuingilia mhimili wa mahakama lakini najiuliza sasa ni takribani miaka minane kesi hii bado iko kwenye upelelezi,” amesema Shafi.

Shafi amehoji “Bado haujakamilika ushahidi wake, je hakukuwa na mamlaka Mahakama kuu Zanzibar kusikiliza kesi hii mpaka isikilizwe Bara? Serikali ituambie nini shida watu hawa hadi leo wanahsikiliwa. Tunahitahji tuwatendee haki Wazanzibari.”

Mwanasiasa huyo amemwangukia Rais Magufuli, akimuomba awasamehe watuhumiwa hao kama alivyowasamehe raia wa Ethiopia zaidi ya 1,000 waliofungwa nchini kutokana na makosa mbalimbali, hivi karibuni.

“Naomba nitumie fursa hii kumuomba rais msikivu, mtetea wanyonge anayesema aombewe, nimuombe kama alivyowaachia wale Waethiopia na wale Wazanzibari na wao awaachie, awahurumie, atumie nafasi yake ya urais kuhakikisha wanatendewa haki,” alisema Shafi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!