Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lazidi kuwakingia kifua waliofukuzwa Chadema
Habari za Siasa

Bunge lazidi kuwakingia kifua waliofukuzwa Chadema

Stephen Kagaigai, Katibu wa Bunge
Spread the love

 

TUHUMA kwamba Bunge la Tanzania nidhaifu zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), zimepingwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Lissu ambaye aligombea urais wa Tanzania Bara kupitia Chadema na kushika nafasi ya pili kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, alitoa madai hayo wakati akizungumza kwe nye mjadala ulioendeshwa televisheni ya mtandaoni tarehe 5 Februari 2021.

Mjadala huo ulibeba kicha cha Habari ‘Je wabunge 19 waliofukuzwa Chadema wanastahili kuwepo bungeni?’

“Nilitaka hii kuweka sawasawa, leo tunazungumza hawa wabunge 19, lakini kinachodhihirisha ni kwamba bunge letu linahitaji kukombolewa, bunge letu ni dhaifu. Ndiyo maana linaingiza yeyote linalomtaka,” alidai Lissu.

Tundu Lissu,

Wabunge hao waliovuliwa uanachama wa Chadema kwa madai ya usaliti ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Halima Mdee, Nusrat Hanje, Grace Tendega , Hawa Mwaifunga na Jesca Kishoa.

Wengine ni Agnesta Lambat, Tunza Malapo, Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu leo tarehe 6 Februari 2021, kuhusu madai ya Lissu, Stephen Kagaigai ambaye ni Katibu wa Bunge amesema “Bunge haliwezi kuwa dhaifu hata siku moja.”

Na hata alipoulizwa Zaidi kuhusu madai ya Lissu, Kagaigai alikataa kutoa ufafanuzi Zaidi “sina cha kuzungumzia kwenye hilo suala. Sina cha kuzungumzia.”

bunge la tanzania

Jana tarehe 5 Februari 2021, Lissu alidai kwamba kitendo cha bunge hilo kuwapokea Mdee nawenzake waliofukuzwa uanachama, kinadhihirisha kwamba mhimili huo ni dhaifu.

Mdee na wenzake walivuliwa uanachama wa Chadema tarehe 27 Novemba 2020, siku tatu baada ya kuapishwa na Spika Job Ndugai, kuwa wabunge viti maalumu.

Mdee na wenzake walituhumiwa kwa makosa ya kusaliti msimamo wa Chadema wa kutopeleka wawakilishi wake bungeni, wakipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, kwa madai kwamba mchakato wake haukuwa huru na wa haki.

Hata hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), zilikanusha madai hayo zikisema kwamba ziliendesha mchakato huo katika misingi ya ukweli, haki na uwazi.

Lissu anayeishi nchini Ubelgiji, alisema ili Bunge hilo liwe imara, ni lazima Katiba ya Tanzania ifanyiwe mabadiliko.

“tatizo hili Bunge kuwa dhaifu litaendelea hadi itakapotatuliwa kwenye mabadiliko makubwa ya kikatiba,” alidai Lissu.

Lissu alisisitiza “ukiwa na mfumo wa urais wa kifalme bunge haliwezi kuwa na nguvu, ili liwe na nguvu lazima kuwe na uwezekano kikatiba wabunge kuingia bungeni bila ya chama cha siasa.”

Akichangia mjadala huo, Godbless Lema, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chadema amesema, wabunge hao hawakupaswa kuwa bungeni baada ya kufukuzwa uanachama na kisha mamlaka husika kupewa taarifa juu ya uamuzi huo.

“Kwa Taifa ambalo linaheshimu misingi ya haki na sheria, hatupaswi hata kuweka kikao cha kuwafukuza, walipaswa wasiwepo hata bungeni.

“Sababu hakuna aliyewatambulisha kama wabunge wa Chadema, hakuna kikao kilichofanyika, na hata tulipopeleka barua kuwa si wabunge bado wameendelea kuwa wabunge,” alisema Lema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!