December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kansiime kuwavunja mbavu Dar

Spread the love

 

WAKATI tukiwa ukingoni kuuhitimisha mwaka huu, Zamaradi Mketema ambaye ni mtangazaji maarufu nchini, atamshusha mchekeshaji bora kutoka Uganda, Anna Kansiime jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kansiime pamoja na wachekeshaji wengine wa nchini Tanzania, Mpoki, MC Pilipili na Mboneke maarufu ‘Irudiwe’ ni miongoni mwao ambao watawavunja mbavu wakazi wa jiji hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zamaradi amesema, onesho hilo alilolipa jina la ‘December to Remember’ litafanyika tarehe 4 Desemba 2021, katika viwanja vya Gymkhana kwa kiingilio cha Sh.200,000 na Sh.2 milioni kwa meza moja ya watu 10.

Zamaradi ambaye ni mratibu wa onyesho hilo, litakuwa onesho la aina yake “lenye hadhi fulani na ndiyo maana hata gaharama zake ni tofauti stand up comedy tulizozizoea. Hii itakuwa ya aina yake na bora sana.”

“Baada ya pilika pilika za mwaka mzima, tunahitaji kufurahia na ndiyo maana tunamleta mchekezaji maarufu Afrika Mashariki kutoka Uganda, Kansiime ambaye atashirikia na wachekeshaji wetu wa hapa nchini kama Mpoki, MC Pilipili na Mboneke na wengine wengi,” amesema

Pamoja na burudani hiyo, “litakuwa ni eneo la makutano, kwa sababu litakuwa ni onesho la hadhi fulani, unaweza kuja na baba yako, mama yako, mjomba au mtoto. Lakini kuongeza connection na watu mbalimbali watakaokuwepo.”

Zamaradi amewaomba wananchi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya karibu, kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo.

error: Content is protected !!