December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kisa katiba mpya: CUF kushitaki Serikali ya Kikwete

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kulia), akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba

Spread the love

 

JUMUIYA ya Vijana Chama cha Wananchi (JUVICUF), inajiandaa kuifungulia kesi Serikali ya awamu ya nne nchini Tanzania kwa madai ya kusababishia nchi hasara ya mabilioni ya fedha kwa kushindikana kupatikana kwa Katiba mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Serikali ya awamu ya nne kati yam waka 2005 hadi 2015 ilikuwa inaongozwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo mwaka 2012, aliruhusu mchakato wa Katiba mpya kuanza baada ya madai ya muda mrefu kutoka kwa wananchi.

JUVICUF inaibuka na hoja hiyo ikiwa ni miaka michache kupita baada ya Mwandishi wa Habari Nguli na Wakili, Jenerali Ulimwengu katika kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kuongozwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa, kusema Rais Kikwete anapaswa kushitakiwa.

Soma undani wa habari hii katika Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Ijumaa tarehe 19 Novemba 2021 kujua zaidi malengo ya JUVICUF.

error: Content is protected !!