Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jussa asema Maalim Seif alipigania kwa dhati umoja na maridhiano
Habari za Siasa

Jussa asema Maalim Seif alipigania kwa dhati umoja na maridhiano

Maalim Seif Sharrif Hamad, Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Spread the love

 

KAIMU Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Maalim Seif Foundation, Ismail Jussa amesema katika mkutano wa mwaka huu wameamua kuupa jina la ‘Maalim Seif, umoja na Maridhiano katika Ujenzi wa Zanzibar na Tanzania mpya,’ kwani katika maisha yake alipigania kwa dhati umoja na maridhiano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Jussa amesema hayo leo tarehe 5 Novemba, 2021 wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa kumbukumbu ya maisha ya Maalim Seif katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip – Zanzibar.

Amesema taasisi hiyo imepata usajili tarehe 29 Oktoba, 2021 hivyo wameona usipite muda mrefu bila kumkumbuka hasa ikizingatiwa miezi iliyopita maambukizi ya Corona yalikuwa yamepamba moto.

“Tukaamua shughuli ya mwanzo ya taasisi hii ni kufanya mkutano huu ambao ni mwanzo wa mikutano ya kila mwaka kumbuka Maalim Seif.

“Mkutano wa mwaka huu tumeona tuupe jina la ‘Maalim Seif, umoja na Maridhiano katika Ujenzi wa Zanzibar na Tanzania mpya,’ tumeamua kuchagua maudhui haya kwa kuanzia kwa sababu katika maisha yake alipigania kwa dhati umoja na maridhiano,” amesema.

Amesema wanakusudia katika taasisi hiyo kuwa na mkutano huo kila mwaka kumuenzi Maalim Seif katika yale aliyosimamia ikiwamo masuala ya demokrasia, umoja, maridhiano, haki, maendeleo, amani na ustawi wa watu wa Zanzibar, Tanzana na duniani.

1 Comment

  • MLIZOWEA KUMCHEZEA NA KUMUONA ZAIF KUTOKANA NA UVUMILIVU WAKE ILA SASA NI WAKATI WA MUAFAKA WA KUTOKUBALI KUDHULUMIWA HAKI ZETU ZA KISIASA RABDA MTUUWE SOTE LAKINI HATUTO KUBALI SABABU MAALIM ALIKUWA ANASHINDA KILA NYAKATI ZA UCHAGUZI MKUU LAKINI MLIKUWA MNATUIBIA KURA NA KUJITANGAZA WASHINDI,KUUWA WANACHAMA WAKE NA KUMWAMBIA NJOO TUUZUNGUMZE, MAZUNGUMZO SASA BASI HAYATOKUWEPO TENA IWAPO MTAENDELEZA UJINGA WA KUTULETEA MAMLUKI NA WIZI WA KURA PAMOJA NA KUUWA WANACHAMA WETU . HATUTOKUBALI N`GOOOOO KUENDELEA KUKAA VIKAO NA NYINYI MAJINI SUBIANI HIVISASA TUPO SEIF VICHAAA SIO TENA SEIF SHARIF HAMAD.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!