August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Isango azikwa kijijini kwao Kisasida

Spread the love

HATIMAYE mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari, Josephat Isango tayari umepumzishwa katika nyumba ya milele kijijini kwao Kisasida mkoani Singida, anaandika Hamisi Mguta.

Isango alifariki Aprili 14 siku ya Ijumaa Kuu katika hospitali ya Ikungi mkoani humo alipokuwa amelazwa kwa wiki mbili akisumbuliwa na tatizo la kupanuka kwa moyo.

Mwandishi huyo aliyekuwa mashuhuri katika kupigania haki za wanyonge amezikwa mita chache kutoka nyumbani kwao.

error: Content is protected !!