Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa ataka riba ya mikopo ipungue
Habari MchanganyikoTangulizi

Majaliwa ataka riba ya mikopo ipungue

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

SERIKALI imeitaka mifuko ya kijamii ambayo inatoa mikopo kwa jamii kufanya marekebisho upya ili kuona uwezekano kupunguza kiwango cha riba, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, alipokuwa akizindua Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi, lililozinduliwa katika viwanja vya mashujaa Dodoma.

Majariwa amesema ili kutekeleza sera ya kumkwamua mwananchi katika hali ya umasikini ikiwa ni kupitia katika mifuko ya kijamii ni vyema sasa mifuko hiyo inafanya mapitio upya kwa lengo la kuangalia ni jinsi gani ya kuweza kupunguza riba.

Amesema kwamba jamii imekuwa haipati ujasiri wa kukopa mikopo kutoka kwenye mifuko ya kijamii kutokana na kuogopa riba kubwa ambayo inatolewa.

Katika hatua nyingine amewataka mawaziri pamoja na wakuu wa mifuko hiyo kuhakikisha anatoa elimu kwa jamii kwa lengo ya kuwapatia mikopo ambayo itawasaidia kuepukana na umasikini.

“Kwa sasa tumezindua baraza hili na ni mara ya kwanza kuzinduliwa rasmi tangu ianzishwe, hivyo basi mifuko hiyo inatakiwa kufanya kazi kwa uwazi kwa malengo ya kusaidia jamii na si vinginevyo.

“Ili kuweza kulifanya taifa kufikia sera ya Tanzania ya viwanda ni lazima kufanya linalowezekana kuhakikisha mwananchi wa kipato cha chini anawezeshwa na si kwa kumwekea riba kubwa katika mkopo au kumwekea masharti magumu,” amesema Majaliwa.

Pamoja na kuwepo mifuko hiyo pia amelitaka baraza la uwekezaji wananchi kiuchumi kufanya tathimini ya kuweza kuiunganisha mifuko hiyo kwa pamoja.

“Nalitaka baraza hili ifikapo Mei 28 mwaka huu nipewe majibu ya nini matokeo ya tathimini ambayo imefanyika kwa ajili ya kuunganisha mifuko ili kuachana na utitiri wa mifuko ambayo ipo kwa sasa,” amesema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Taifa la Kiuchumi, Dk. John Jingu amesema jitihada sera ya serikali kuwa ya viwanda haziwezi kufanikiwa endapo hapatakuwa na ushirikiano kati ya serikali na wafanyabiashara.

Amesema kuwa moja ya vikwazo vya kutokufikia malengo kwa wananchi ni ukosefu wa mitaji, hivyo basi kwa kuwa mkuu wananchi kadhamilia kulifanya taifa kuwa na uchumi wa kati ni lazima wananchi wawezeshwe.

“Mifuko hii inatakiwa kujipanga na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na kila mfuko uhakikisha unajenga kiwanda angalau kimoja katika maeneo yao ya kazi,” amesema Dk. Jingu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!