Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko IGP Sirro apangua makamanda wa mikoa
Habari Mchanganyiko

IGP Sirro apangua makamanda wa mikoa

Spread the love

MKUU wa jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro, ametangaza mabadiliko ya makamanda wa mikoa katika jeshi lake kwa kuhamisha baadhi huku na kupeleka kule. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Miongoni mwa waliohamishwa, ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishena, Ahmed Msangi ambaye ameletwa makao makuu ya upelelezi jijini Dar es Salaam.

Msangi amefanywa kuwa mkuu wa kitengo cha makosa dhidi ya binadamu.

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa leo tarehe 15 Agosti 2018 na msemaji wa jeshi hilo, Kamishena msaidizi wa polisi, Barnabas Mwakalukwa.

“Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Sehemu ya taarifa hiyo pia imeeleza kuwa  nafasi ya DCP Msangi, imechukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shana.

Naye aliyekuwa mkuu wa operesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Wankyo Nyigesa, amechukua nafasi ya Shana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!