Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko GGML yaibuka muonyeshaji bora katika maonyesho ya OSHA- 2023
Habari Mchanganyiko

GGML yaibuka muonyeshaji bora katika maonyesho ya OSHA- 2023

Spread the love

KATIKA maadhimisho ya siku ya afya na usalama mahali pa kazi  yanayoratibiwa na Wakala wa afya na usalama mahali pa kazi (OSHA), Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetangazwa muonyeshaji bora (Overall best exhibitor) miongoni mwa kampuni zote zilizoshiriki maonyesho hayo mjini Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo Afisa Uhusiano wa GGML, Doreen Denis baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi ya kundi la muoneshaji bora katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea mkoani Morogoro.

Pia imetangazwa kuwa mbunifu bora wa maonesho hayo yaliyoanza Aprili 26 na kutarajiwa kuhitimishwa Aprili 30 mwaka huu katika viwanja vya Tumbaku mkoani humo.

Kilele cha maonesho hayo yenye kauli mbiu Mazingira Salama na Afya ni Kanuni na Haki ya Msingi Mahali pa Kazi.” kimefanyika jana mkoani humo.

Afisa Uhusiano wa GGML, Doreen Denis (kushoto) akimfafanulia jambo mwananchi aliyetembelea banda la maonesho la kampuni hiyo katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro. Wapili kushoto ni Afisa Mawasiliano Afisa Mawasiliano mwandamizi wa GGML, Laurian Theophil Pima.
Daktari wa Kituo cha Afya cha GGML kutoka Idara ya Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo ya GGML, Dk. Subira Joseph akitoa huduma za matibabu kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la huduma za afya la kampuni hiyo kwenye maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayofanyika mkoani Morogoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

error: Content is protected !!