Wednesday , 22 May 2024
Home Kitengo Biashara GGML ilivyong’ara usiku wa madini, yatwaa tuzo 2
Biashara

GGML ilivyong’ara usiku wa madini, yatwaa tuzo 2

Spread the love

Mchango wa Kampuni ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited (GGML) umeendelea kutambuliwa na wadau mbalimbali wa sekta ya madini kupitia Kongamano la Kimafaifa la Uwekezaji na Madini Tanzania 2023 kutokana na jitihada zake katika uwajibikaji kwa jamii pamoja na kuzingatia afya na usalama mahala pa kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang’anamuno (kushoto) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika kipengele cha uhifadhi mazingira, afya na usalama mahala pa kazi, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Hafla hiyo iliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inatokana na Kampuni hiyo kushinda tuzo mbili ambazo ni mshindi wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) pamoja na uhifadhi wa mazingira, afya na usalama kazini. Tuzo hizo zilizotolewa na Wizara ya Madini  zimeendelea kudhihirisha hadhi ya GGML kuwa mfano wa kuigwa katika masuala hayo ya afya na usalama kazini pamoja na kukuza uchumi wa Taifa.

Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang’anamuno (kushoto) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR), Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Hafla hiyo iliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Madini wa Serikali ya Malawi, Monica Chang’anamuno akiongozana na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alikabidhi tuzo hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong pamoja na Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo.

Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang’anamuno (mwenye nguo nyekundu katikati) akiwa amebeba tuzo yake ya heshima ya ushiriki wa kongamano la Kimataifa la Madini na Uwekezaji Tanzania 2023. Wengine ni viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) walioshiriki katika hafla ya usikun wa madini.

Hafla hiyo iliyopewa jina la Usiku wa Madini, ilifanyika tarehe 25 Oktoba 2023 jijini Dar es salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

BiasharaElimu

Benki ya Exim yazindua huduma ya ‘Exim Smart Shule’

Spread the love  KATIKA juhudi za kuboresha teknolojia za kidijitali katika sekta...

Biashara

Shinda mkwanja Meridianbet Kasino, ukicheza Expanse Tournament.

Spread the love  LION Kingdom ni sloti kutoka kasino ya mtandaoni yenye...

Biashara

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

error: Content is protected !!