October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

FIFA: Ya Sepp Blatter yamkuta Infantino

Spread the love

TUHUMA za rushwa ndani ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), limechepua tena na sasa Gianni Infantino, rais wa shirika hilo amefunguliwa jalada la uchunguzi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Infantino anatuhumiwa kuingilia uchunguzi uliofanywa na FIFA dhidi ya Sepp Blatter mwaka 2015, aliyekuwa rais wa shirika hilo kwa kutoa taarifa za uongo na kwa maslahi binafsi. Infantino aliapishwa kuwa rais wa FIFA tarehe 26 Februari 2016.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Uswisi Stefan Keller, wiki iliyopita, Infantino alifunguliwa jalada la uchunguzi kuhusu kuhusika kwake, ni baada ya kuonekana kuwepo kwa viashiria vya Infantino kufanya vigisu wakati wa uchunguzi wa Blatter.

Hata hivyo, Infantino amepuuza madai hayo ambayo sasa yanaripotiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya habari vya Uswisi na Ujerumani.

error: Content is protected !!