Monday , 11 December 2023
Habari za SiasaTangulizi

Ngoma bado mbichi CCM

Spread the love

KAULI ya Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu na Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwamba ‘wateule hawajapatikana,’ inaumiza vichwa waliopitishwa kwenye kura za maoni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kila mmoja kwa wakati wake amesema, kilichofanywa kwenye kura za maoni na hatimaye wateule wa ubunge, udiwani na uwakilishi kupatikana, ni msaada wa kuonesha picha ya hali ilivyo kwenye maeneo hayo.

Na kwamba, kile kilichoamuliwa na wajumbe kwenye maeneo hayo, kinaweza kupitishwa na Kamati Kuu ya chama hicho ama kupinduliwa.

Kwa muktadha huo, si aliyeshinda kwenye mchakato wa kura za maoni ya ubunge na udiwani wala aliyeshindwa, kila mmoja bado anayo nafasi.

“Mchakato unaendelea, tunakuombea sana basi kile kikao cha mwisho kikurudishe, lakini waliokupa ni wajumbe, wametoa mwongozo tu.

“Maamuzi yako juu huko, tunaamini In Sha Allah kule Handeni utakuwa mbunge. Tunakuombea,” alisema Majaliwa akimweleza Hussein Msopa (Shehe Sharif Majini) wakati akizungumza kwenye Baraza la Eid Ijumaa tarehe 31 Julai 2020.

Msopa amepitishwa kwenye Jimbo la Handeni Vijijini, na sasa anasuburu uamuzi wa vikao vya Kamati Kuu.

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wakati Waziri Majaliwa akitoa kauli hiyo, Polepole amesema Ibara ya 67 ya katiba ya chama hicho, inaipa nguvu Kamati Kuu kufanya uamuzi wake binafsi hata bila kutegemea mchakato uliofanywa na wajumbe katika kupendekeza majina hayo.

Polepole akizungumza kwenye kipindi cha Mizani cha Televisheni ya Taifa (TBC), alisema mchakato wa awali unaonesha taswira tu na kwamba, Kamati Kuu ndio inatoa uamuzi wa mwisho.

Tayari Kamati za Wilaya za Siasa CCM zinaendelea kufanya kazi yake ikiwa kujadili majina ya wagombea na kisha kweka mapendekezo yao yakiambatana na sababu za kupendekeza majina hayo.

Willium Ngereja (katikati)

Pia Kamati ya Siasa ya Mkoa, yenyewe ina wajibu wa kujadili pia majina yaliyopendekezwa na Kamati ya Wilayaya Siasa na kuambatanisha sababu za kukubali mapendekezo hayo ama kukataa.

Kauli ya Polepole na Majaliwa hiyo inaashiria kwamba, si kila aliyepitishwa na wajumbe walipoiga kura kwa ajili ya kupendekeza jina la mbunge, diwani na wawakilishi wateule, wanaweza kurejeshwa na Kamati Kuu, lolote limaweza kutokea.

Polepole amefafanua, majina yaliyopendekezwa kwenda Kamati Kuu Majina, yatapitiwa ikiwa ni pamoja na taarifa za wenye majina hayo huku suala la uadilifu, utii na usalama vikishika hatamu kwenye mjadala huo.

Askofu Josephat Gwajima

Kwa mujibu wa Polepole, leo tarehe 2 Agosti 2020, ni siku ya pili ya vikao vya Kamati za Siasa za CCM wilaya kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa kamati za siasa za mkoa.

Ratiba inaonesha Jumanne tarehe 4 – 5 Agosti 2020, kutakuwa na vikao vya kamati za siasa za Mkoa kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa vikao vya juu.

Amesema, mchujo unazingatia pamoja na mambo mengine, pia sifa za msingi za kiongozi kwenye chama kama zinavyoanishwa na katiba na kanuni ikiwamo kutosheka, kutotawaliwa na tamaa.

1 Comment

  • Yetu macho wapinzani muingize wagombea wawili jimbo moja na wagombea uraisi wawili badala ya kumsapoti mmoja kwa ajili ya ubinafc wenu mtachekesha na hatutawaamini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!