Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu kupenya Urais Chadema?
Habari za Siasa

Lissu kupenya Urais Chadema?

Spread the love

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ndio jina linalokita kwenye vichwa vya wengi kuhusu kupitishwa kwake kuwania urais wa Tanzania Bara. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam..(endelea).

Kamati Kuu ya chama hicho, imekutana leo tarehe 2 Agosti 2020, kujadili na kutathmini majina ya wagombea urais kwa ajili ya hatua zingine kuelekea kumpata atakayewakilisha chama hicho kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Lissu ni miongoni mwa majina saba ya wanasiasa wa chama hicho waliojitokeza kuchukua, kujaza na kurejesha fomu ya kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.

Majina mengine ni Wakili Simba Neo, Lazaro Nyalandu, Wakili Gasper Mwanalyela, Isaya Mwita, Mchungaji Leonard Manyama na Dk. Myrose Majinge.

Lissu ambaye amerejea nchini tarehe 27 Julai 2020, ni miongoni mwa watia nia waliohudhuria kikao hicho kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mliman Citty, jijini Dar es Salaam.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa ndiye anayeongoza jopo la kamati hiyo akiwemo Tundu na Lazaro Nyarundu ambaye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Kati. Nyalandu na Lissu ambao ni wajumbe wa kamati hiyo, wote ni watia nia.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema Taifa

Tumain Makene, Ofisa Habari wa chama hicho akitoa taarifa kuhusu kikao hicho leo, amesema Kamati Kuu inaketi na kupitia pia kutafiti majina ya wagombea kabla ya kuyapeleka Baraza Kuu la chama.

Amesema, baraza hilo litakutana kesho tarehe 3 Agosti 2020 na kupitia majina, kisha majina yatapelekwa kwenye Mkutano Mkuu utakaofanyika tarehe 4 Agosti 2020 kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea wa urais wa chama hicho.

Amesema, Kamati Kuu inayoketi leo itajadili majina ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Tanzania na mgombea Urais wa Zanzibar sambamba na wagombea wenza.

“Kamati Kuu ina wajibu wa kufanya utafiti wa wagombea watakaochaguliwa kupeperusha bendera ya chama chetu,” amesema Makene.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!