Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Fei Toto ampa zawadi ya mabao Niyonzima
MichezoTangulizi

Fei Toto ampa zawadi ya mabao Niyonzima

Feisal Salum 'Fei Toto' kiungo wa klabu ya Yanga
Spread the love

 

KIUNGO wa klabu ya Yanga, Feisal Salum ambaye ndiye mfunga wa mabao yote mawili kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Ihefu na kutumia mabao hayo kama zawadi ya kumuaga Haruna Niyonzima ambaye anaachana na klabu hiyo baada ya msimu huu kukamilika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania ulifanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, majira ya saa 10 jioni.

Mara baada ya kufunga mabao hayo mawili kwenye dakika ya 17 na 36 Feisal alisema kuwa mabao hayo ya leo amemzawadia Niyonzima kwa kuwa ameishi naye vizuri.

“Nilichomwandalia Haruna kwenye mchezo wa leo ni zawadi ya mabao, nimeishi naye vizuri na amekaa kwenye soka la bongo muda mrefu,” alifunguka Feisal.

Kwenye mchezo huo, Niyonzima aliingia uwanjani kwenye dakika 60 kwa kuchukua nafasi ya Zawadi Mauya na kutumia dakika 30 tu, kucheza mchezo wa mwisho na timu hiyo wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Mara baada ya mchezo huo kukamilika Niyonzima alisema kuwa, amefurahi kuachana na Yanga kwa heshima kubwa, nikiwa salama toka alipofika nchini msimu wa 2011/12 akitokea Rwanda.

“Nashukuru nimekuja Tanzania toka msimu wa 2011/12, nikiwa mzima na leo nimemaliza nikiwa mzima, nimeachana na timu yangu kwa uzuri na heshima kubwa, nimejivunia kuwafanya watu wa Rwanda wote kuipenda Yanga,” alisema Haruna

Aidha mchezaji huyo aliendelea kusema kuwa kwa sasa bado hajaachana na mpira ila anaondoka ndani ya klabu ya Yanga kwa kuwa yeye bado ni mchezaji.

Haruna Niyonzima

“Nitakumbuka mapenzi ya mashabiki wa Yanga na watanzania, naondoka kwenye klabu ya Yanga, lakini bado ni mchezaji, nina kumbumbuku nyingi sana itakayonifanya nirudi na kuishi hapa,” aliongezea Haruna.

Niyonzima kwa mara ya kwanza alikuja nchini akitokea Rwanda kwenye klabu ya APR msimu wa 2011/12 na kucheza Yanga mpaka msimu wa 2017, kisha alitimkia kwenye klabu ya Simba na mwaka 2020 alirejea tena Yanga.

Mchezaji huyo ameshinda jumla ya mataji sita ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya hayo manne alitwaa akiwa na Yanga na mawili akiwa na Simba SC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!