Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Waganga 16 mbaroni, wengine wasakwa
Habari Mchanganyiko

Waganga 16 mbaroni, wengine wasakwa

Sehemu ya vifaa vya waganga wapiga ramli
Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda ya Magharibi, limewakamata waganga wa kienyeji 16, wanaotuhumiwa kufanya shughuli zao kinyume cha sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 15 Julai 2021 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Katavi, ACP Benjamin Kuzaga, kwa niaba ya makamanda wa Jeshi la Polisi wa mikoa ya kanda hiyo, ikiwemo Tabora na Kigoma.

Kamanda Kuzaga amesema, watuhumiwa hao walikamatwa katika operesheni maalumu ya kusaka wahalifu, iliyofanyika kuanzia tarehe 9 Juni hadi 14 Julai mwaka huu.

Amesema waganga 10 wanatuhumiwa kufanya kazi bila vibali, huku sita wakituhumiwa kupiga ramli changamoto.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Katavi, ACP Benjamin Kuzaga

“Tumewakamata watu wanaojihusisha na ramli chonganishi, hawa bado wanazidi kwanza wanatumia nyara za Serikali, lakini pia wanadanganya watu. Hii inasababisha kutokea mauaji yasiyo kawaida,” amesema Kamanda Kuzaga.

Kamanda Kuzaga amesema, katika operesheni hiyo, Polisi waliwakamata watuhumiwa 292, ikiwemo 100 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya pombe haramu ya gongo na 133 wanaotuhumiwa kwa makosa ya uhamiaji haramu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 120 za DMDP zaibadilisha Ilala, wananchi watoa ya moyoni

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 120.7 zimetumiwa na Halmshauri ya Jiji...

error: Content is protected !!