Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ester Bulaya amtaka ‘waziri wa kikokotoo ang’oke’
Habari za SiasaTangulizi

Ester Bulaya amtaka ‘waziri wa kikokotoo ang’oke’

Spread the love

MBUNGE wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amemtaka Rais John Magufuli kumfukuza kazi Waziri wa Sera, Bunge, Ajira, Vijana, na Walemavu, Jenista Mhagama, kwa sababu ya kutunga kanuni mpya ya kikokotoo cha mafao ya wastaafu ambayo ilikuwa mwiba kwa wafanyakazi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mwishoni mwa mwaka jana Rais Magufuli alifuta kanuni hiyo ambayo ilikuwa inaelekeza wastaafu kulipwa asilimia 25 ya mafao yao wanapostaafu na asilimia 75 inayobakia kila mwezi, na kuagiza kikokotoo cha zamani cha malipo ya asilimia 50 ya mafao wanapostaafu, na asilimia 50 inayobakia kila mwezi kitumike katika kipindi cha mpito hadi mwaka 2023.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 2 Januari 2019, Bulaya ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, amesema Waziri Jenista ndiye alipigia debe kanuni hiyo bungeni, na kumtaka kujiuzulu mwenyewe .

“Morali kazini zimeshuka sababu ya mtu mmoja halafu bado yupo ofisini is not fair ‘sio haki’. Dada yangu namheshimu ila anapaswa kuwajibika katika hili sina chuki nae,” amesema Bulaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!