July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dube, Sure Boy kuikosa Simba

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Azam FC, Prince Dube pamoja na kiungo wa klabu hiyo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wataokusa mchezo dhidi ya Simba mara baada ya kupata majeruhi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utapigwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi majira ya saa 1 usiku.

Akithibitisha kukosekana kwa wachezaji hao, kocha msaidizi wa klabu hiyo, Vivier Bahati amesema kuwa wachezaji hao pamoja na Aggrey Morris watakosekana kutokana na sababu za kiafya.

“Katika mchezo wa kesho, tutamkosa mshambuliaji wetu Prince Dube anayesumbuliwa na majeruhi, pia kiungo wetu Sure Boy ambaye amepata homa pamoja na nahodha, Agrrey Morris,” alisema kocha huyo.

Azam FC wanaingia kwenye mchezo huo, huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa bao 1-0, kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye ligi, timu hizo zilifungana mabao 2-2.

error: Content is protected !!