Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Drone kutumika ulinzi wa bomba la TAZAMA
Habari MchanganyikoTangulizi

Drone kutumika ulinzi wa bomba la TAZAMA

Spread the love

NDEGE ndogo zisizo na rubani (drone) zinatarajiwa kutumika katika ulinzi wa bomba la mafuta linalotumika kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Dar es Salaam – Tanzania hadi Ndola – nchini Zambia lijulikanalo kama TAZAMA.

Mbali na drone, pia wanakijiji ambao bomba hilo lililojengwa miaka ya 1960 linapita, wanatarajiwa kushirikishwa kikamilifu katika ulinzi wa bomba hilo ambalo tangu Januari mwaka huu linasafirisha mafuta ya dizeli badala ya mafuta ghafi ambayo yalipigwa ‘stop’ na Serikali ya Tanzania. Anaripoti Gabriel Mushi…(endelea).

Waziri wa Nishati, January Makamba

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam leo tarehe 7 Julai 2023 Waziri wa Ulinzi wa Zambia, Ambrose Lufuma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika kikao cha mawaziri sita wa Tanzania na Zambia.

Kikao hicho cha pili kilichofanyika jijini Dar es Salaam kimejumuisha Waziri wa Nishati, Januari Makamba; Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni; Waziri wa Ulinzi, Innocent Bashungwa.

Kwa upande wa Zambia walioshiriki pamoja Lufuma, Waziri wa Mambo ya Ndani, Jack Mwiimbu na Waziri wa Nishati, Peter Kapala.

Lufuma amesema polisi wa pande zote mbili watatumia ndege hizo zisizo na rubani zilizo katika hatua ya mwisho ya usajili, kwa upande wa Tanzania na Zambia.

Aidha, akizungumzia kikao hicho, Waziri wa Nishati, January Makamba amesema bomba hilo la TAZAMA lenye urefu wa Km 1,710 kutoka Kigamboni-Dar es Salaam hadi Ndola- Zambia, linatarajiwa kupanuliwa ili kukidhi mahitaji ya mafuta katika soko la Zambia na baadhi ya mikoa ya Tanzania

Makamba amesema Serikali za Tanzania na Zambia mbali na kufanya mazungumzo jinsi ya kujenga bomba jipya la mafuta pia zimepanga kujenga bomba jipya la gesi asilia ili kutekeleza malengo ya Tanzania kuiuzia Zambia gesi asilia.

Waziri wa Ulinzi Zambia, Ambrose Lufuma

Kikao hicho cha mawaziri kulitanguliwa na kikao cha makatibu wakuu wa wizara pamoja na watalaam na kujadili mapendekezo ya timu ya watalaam kuhusu taratibu za kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa bomba jipa la mafuta na bomba jipya la gesi asilia.

Amesema miradi hiyo ni mikubwa na muhimu ya kimkakati nchini kwa sababu bomba la mafuta kutoka Kigamboni hadi Ndola Zambia linasafirisha lita milioni 90 za mafuta ya dizeli kwa mwezi.

“Tukijenga bomba kubwa zaidi bandari itapata soko kubwa kwa mafuta yanayoenda Zambia na Kongo, lakini pia itasaidia mikoa ya kusini mwa Tanzania kupata mafuta kwa unafuu kwa sababu kwenye bomba jipya kutakuwa na matoleo ya kushusha mafuta katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Mbeya na Songwe.

“Barabarani kutakuwa na magari machache zaidi na gharama za usafirisihaji zitakuwa chini zaidi, ndio maana kikao hiki ni muhimu kitajadili na kutoa maamuzi kuhusu kuendelea kwa mipango ya upembuzi yakinifu na upatikanaji wa fedha na masuala ya kiufundi katika ujenzi wa bomba hilo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!