April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Vincent Mashinji azomewa kortini

Spread the love

DAKTARI Vincent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kabla ya kujiunga Chama cha Mapinduzi (CCM), amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzomewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Leo tarehe 10 Machi 2020, Dk. Mashinji alikutana na zogo wakati anaingia katika chumba cha mahakama hiyo, kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya Kesi ya Uchochezi Na.112/2018, inayomkabili na viongozi wakuu wa Chadema.

Alipokuwa anaingia katika chumba cha mahakama hiyo, Dk. Mashinji alianza kuzomewa na baadhi ya wafuasi wa Chadema.

Hata hivyo, alivyoingia Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, shangwe ziliibuka huku watu wakiimba ‘Mwamba tuvushe’.

Muda huu watu wanaanza kuingia katika chumba cha mahakama kwa ajili ya kusubiri hukumu ya viongozi hao.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Halima Mdee, Mwenyekiti Bawacha.

error: Content is protected !!