Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Nshalla aonya wanaotaka kumuua kisa bandari
Habari MchanganyikoTangulizi

Dk. Nshalla aonya wanaotaka kumuua kisa bandari

Dk. Rugemeleza Nshalla,
Spread the love

ALIYEKUWA Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Dk. Rugemeleza Nshalla, amewataka watu anaodai wanapanga kumuuwa waache mara moja, kwa kuwa wakifanya hivyo watateseka pamoja na familia zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mwanasheria huyo maarufu nchini, ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Julai 2023, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu madai ya vitisho vya uhai wake.

Amedai  vitisho hivyo vimeibuka kufuatia msimamo wake  wa kukosoa mkataba wa uwekezaji wa bandari ulioingia kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai.

“Naipenda Tanzania, nitaifia nchi yangu, damu yangu ikimwagika iendelee kumwagilia rasilimali za nchi yetu na hao watakaofikiria hayo yatawakuta mabaya kwao. Nawasihi watubu  wafahamu kwamba, siku ya mwisho watajibu sio kwao bali kwa familia zao na vizazi vyao 440 vya familia zao,” amesema Dk. Nshalla.

Dk. Nshalla amesema “kuanzia Sasa zitateswa na zitateseka kwa dhambi hiyo wanayoifanya. Nayasema haya nikiwa na moyo mweupe lakini ndugu zangu kama ndio mwisho wangu nasema kwaherini tutaonana paradise.”

Mwanasheria huyo amedai kuwa, kama madai aliyotoa kuhusu mkataba huo wa kiserikali unaotarajiwa kutekelezwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Serikali ya Dubai kupitia kampuni ya Dubai Port World, ni ya uongo, Mungu achukue uhai wake.

“Nimekuja hapa kama mtanzania na nashikilia imani yangu, nasema nilichokisema kama Mungu anaona ni uongo kwa kushika Biblia hii nianguke chini niondoke duniani. Sisemi Mungu nisaidie bali nasema kama niliyosema ya uongo naomba uhai wangu Mungu auchukue. Mimi mkristo mkatokiki kwa miaka yangu 57 nimeyaona mengi,” amesema Dk. Nshalla.

Amedai, msimamo wake wa kukosoa mkataba huo, ameutoa kwa minajili ya kutimiza matakwa ya katiba ya nchi, hususan Ibara ya 26(1) inayoagiza kila mtanzania kulinda rasilimali za nchi.

“Napenda kusema haya tunayoongea sio kelele, tunasema kwa uchungu kuipinga rasilimali ya nchi yetu kuporwa au kugawiwa  bure kwa watu wengine tunaoaminishwa kuwa wawekezaji kumbe mwisho wa siku ni wachukuaji,” amesema Dk. Nshalla.

Serikali ya Tanzania katika nyakati tofauti imetoa ufafanuzi kuhusu mkataba huo, ikisema haulengi kuuza bandari za nchi kwa DP World, bali unalenga kuboresha utendaji wake hususan katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa kuimarisha mifumo yake ya utendaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!