Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mwinyi: Nitakuja na staili ya Rais Magufuli
Habari za Siasa

Dk. Mwinyi: Nitakuja na staili ya Rais Magufuli

Spread the love

DAKTARI Hussein Ali Mwinyi, Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar,  Oktoba 2020, ameahidi kufuata nyayo za Rais John Pombe Magufuli, katika mapambano ya rushwa, uzembe na ubadhirifu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Dk. Mwinyi ametoa ahadi hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika leo Jumamosi tarehe 11 Julai 2020, jijini Dodoma wakati akiwasalimia wajumbe hao.

Waziri huyo wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa amesema, endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, upole wake atauweka pembeni na kufuata ukali wa Rais Magufuli, katika kushughulikia wala rushwa, wabadhirifu na watumishi wazembe.

“Wako waliosema mimi ni mpole, lakini nimejifunza kutoka kwako mambo ya msingi, rushwa, uzembe na ubadhirifu yanataka uwe mkali na hilo nawaahidi endapo nitachaguliwa kuwa rais, nitakuja na staili ya Rais Magufuli katika maeneo hayo,” ameahidi Dk. Mwinyi .

Dk. Mwinyi amesema, endapo atafanikiwa kuwa Rais wa Zanzibar, atakuwa kiongozi bora kutokana na uzoefu alioupata akiwa waziri chini ya Rais Magufuli na marais wastaafu.

“Katika kipindi hiki cha miaka mitano ya Rais Magufuli, ameendelea kuwa nami kama waziri wake wa ulinzi, jambo limenifanya niwe nakamilisha miaka 11 kama waziri wa ulinzi.”

“Niseme pia nimejifunza mengi kutoka kwako, umenifanya nijifunze mengi katika uongozi na nidiriki kusema huko ninakokwenda nitakuwa kiongozi bora kwa sababu ya kujifunza kwako,” amesema Dk. Mwinyi.

Aidha, Dk. Mwinyi amewashukuru marais wastaafu, Jakaya Kikwete, Benjamini Mkapa na Baba yake, Ali Hassani Mwinyi kwa kumuamini na kumpa nafasi ya juu ya uongozi katika serikali zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!