WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamemthibitisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea Urais wa Tanzania kwa asilimia 100 katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).
Shughuli hiyo ya upigaji kura imefanyika leo Jumamosi tarehe 11 Julai 2020 jijini Dodoma.
Akitangaza matokeo hayo, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema, wajumbe wa mkutano huo ni 1822 na waliopiga kura walikuwa 1822.
Spika Ndugai amesema, hakuna kura hata moja iliyoharibika.
Amesema, kura halali zilikuwa 1822, “kura halali ni 1822. Kura za ndiyo ni 1822 ambayo ni sawa na asilimia 100 ya kura zote. Hakuna kura ya hapana.”
Leave a comment