Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro
Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the love

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia ni Diwani wa kata ya Olbalbal iliyopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, Emmanuel Tonge ni miongoni mwa wananchi 463 waliohama kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera na maeneo mengine. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hafla ya kuwaaga wananchi wanaohama kwa hiari imefanyika leo tarehe 19 machi, 2024 na kuongozwa na mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Kanali Wilson Sakulo ambapo jumla ya kaya 77 zenye watu 463 na mifugo 1,408 wamehama ndani ya hifadhi hiyo baada ya kujiandikisha kuhama kwa hiari.

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia ni Diwani wa kata ya Olbalbal iliyopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, Emmanuel Tonge.

Diwani wa kata ya Olbalbal ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngorongoro na katibu wa baraza la wafugaji Ngorongoro amesema ameamua kuhama baada ya kuona dhamira ya Serikali ya awamu ya 6 kuboresha huduma bora za kijamii nje ya hifadhi na kurahisisha mazingira ya uandikishaji kwa kuwafuata wananchi kwenye ofisi za vitongoji, vijiji na kata kuwapatia elimu ya kutosha kuhusu uwepo wa maisha bora ndani ya hifadhi.

“Ndani ya hifadhi hakuna kesho iliyobora kwa watoto wangu, Serikali ikaona itenge maeneo rasmi na kujenga huduma za kijamii kama shule, vituo vya afya, zahanati, maji safi, barabara, mawasiliano ya simu, posta, majosho, eneo la malisho na mashamba ya kutosha kwa kilimo, kwa fursa hii sina haja ya kuendelea kushi na Wanyama ndani ya hifadhi” ameongeza Tonge.

Meneja mradi wa kuhamisha wananchi wanaohama kwa hiari Ngorongoro Afisa Uhifadhi Mkuu Flora Assey ameeleza kuwa hadi kufikia wiki hii jumla ya kaya 1,195 zenye watu 7,195 na mifugo 33,064 zimeshahama ndani ya Hifadhi.

Ameongeza kuwa kati ya kaya 77 zilizohama ndani ya hifadhi wiki hii, kaya 75 zimeenda Kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni na kaya mbili (02) zimehamia kijiji cha Makao Meatu Mkoani Simiyu.

Naibu Kamishna wa Hifadhi huduma za Shirika NCAA, Salum Mjema amebainisha kuwa Serikali imeendelea kuboresha zoezi la utoaji elimu, uandikishaji na uthaminishaji  kwa kuongeza timu ya uandikishaji ambapo ndani ya mwezi mmoja taratibu zote ikiwepo malipo zinakuwa zimekamilika na wananchi kuhamishwa bila kusiburi mda mrefu.

Mjema ameongeza kuwa ujenzi wa nyumba za makazi 2,500 katika Kijiji cha Msomera unaendelea kwa kasi  ambapo nyumba 903 zimeshakamilika, nyumba 97 zipo katika hatua za umaliziaji, nyumba 1500 zipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi huku maandalizi ya ujenzi wa nyumba zingine 2500 yakiendelea katika vijiji vya Kitwai Wilani Simanjiro na Saunyi wilaya ya Kilindi.

Katika hatua nyingine mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Kanali Wilson Sakulo ametoa wito kwa jamii kupuuza baadhi ya watu wanaopotosha kuwa baadhi ya wananchi wanaohamishwa ndani ya hifadhi sio wakazi wa Ngorongoro.

Amesisitiza kuwa serikali iko macho na makini katika utekelezaji wa zoezi kwa  kuhakikisha wananchi wote wanaojiandikisha kuhama kwa hiari ni wakaazi wenyeji wanaoishi ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro lenye vijiji 25 na kata 11 na si vinginevyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!