October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DC Katambi awachimba mkwara wapinzani kuhoji ulinzi wa Rais

Spread the love

PATROBAS Katambi, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma amesema, watu wanaohoji ulinzi wa rais hawana nia njema. Anaripoti Hamis Mguta… (endelea).

Na kwamba, watu hao kama wangehoji ulinzi alionao Rais John Magufuli wakiwa Dodoma, angewakamata na kuwatia ndani.

Akizungumza na MwanaHALISI Online ofisini kwake jijini humo amesema, viongozi wa serikali hawapo tayari kumwangusha rais kwa lolote.

“Hatupo tayari kumuangusha Rais Magufuli kwasababu amefanya mambo makubwa. Eti unakuta kuna wapumbavu nasikia wanauliza kwanini rais ana ulinzi mkubwa? ni upuuzi,” amesema.

Katambi ameeleza kuwa, kwa sasa hakuna tajiri anayeweza kuvunja sheria kwasababu ni tajiri na kwamba, hiyo inatokana na rais kuwachukulia hatua mapema.

Bila kumtaja jina Katambi amesema, “huku ni kufilisika kwa hoja, tunawaona wengine walikuwa na watu wanaitwa Red bridged, vijana wengi halafu wanawashindisha na njaa, hawawapi hata chakula, mbona wao hatuwaulizi? Na mimi nilikuwa huko na ninafahamu vijana wale walikuwa wanafanya kazi kwa moyo sana.

“Kiongozi alikuwa na walinzi zaidi ya saba na alikuwa anawashindisha njaa, akishamaliza mambo yake utasikia ‘Komaa Kamanda” halafu anapanda V8 anaondoka, nyie mnatembea kwa miguu,” amesema.

Katambi alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea chama kikuu cha upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jumanne ya tarehe 21 Novemba 2017.

Akiwa Chadema, alikuwa Mwenyekiti wa Barza la Vijana la chama hicho (Bavicha).

error: Content is protected !!