Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kuwaweka raia mahabusu; DC, Waziri wavutana
Habari za Siasa

Kuwaweka raia mahabusu; DC, Waziri wavutana

George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Spread the love

AGIZO la kuzuia kuwaweka watu mahabusu lililotolewa na George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora limepata upinzani. Anaandika Regina Mkonde … (endelea).

Gift Msuya, Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Tabora ameonesha kutokubaliana na agizo hilo akitoa hoja kwamba, ni bora wakuu wa mikoa na wilaya waachwe watekeleze sheria ya kumweka mtu ndani saa 24 kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ya mwaka 1997.

Akiwa kwenye mahojiano na kituo cha radio hapa nchini Msuya amesema kuwa, ‘Ngoma usiyoicheza huwezi jua utamu wake’ na kuwa, hulazimika kutekeleza sheria hiyo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Tarehe 15 Aprili 2019 akiwa bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuchika alikazia marufuku ya serikali kwa wateule hao wa Rais John Magufuli, kutoweka watu mahabusu kinyume cha sheria.

Mkuchika alisisitiza kwamba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi ametoa waraka kwa viongozi hao kuhusu kukazia marufuku hiyo.

Na kwamba, Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya yeyote atakayefunguliwa kesi kuhusu kumuweka mahabusu raia kinyume na sheria, Jamhuri haitamtetea mahakamani.

Msuya amesema “watuache sababu sheria inaturuhusu, na sisi mheshimiwa rais alituteua tukiwa na akili timamu, tunajua tunachofanya. Hatuwezi kufanya kwa kumuonea mtu, siku zote lazima kuna sababu za kufanya hivyo.

“Mimi kama binadamu sifurahii kukaa ndani na sifurahii kumuweka mtu ndani, lakini ninamuweka mtu ndani kwa sababu za msingi.”

Msuya amekiri kuwahi kumuweka mkandarasi wa mradi wa maji wilayani Uyui mahabusu kwa saa 48, kutokana na mkandarasi huyo kugoma kulipa vibarua wake ujira wao.

“Nimeshaweka ndani sio mmoja tu, ni zaidi ya mmoja. Hili suala linasaidia, unajua wanasema ngoma ambayo huichezi, huwezi jua utamu wake, kwa hiyo sisi ambao tunacheza tunajua utamu wake.

“Kwa mfano, katika mradi wetu wa maji tumekuwa na vijana ambao sasa wamegeuka kuwa vibaka kwa sababu hawalipwi malipo yao kwa wakati na mkandarasi aliyewaajiri,” amesema.

Msuya ameeleza kuwa, aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona baadhi ya vibarua wasiolipwa ujira wao, kuanza kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo uporaji kwa ajili ya kujipatia chochote kitu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!