October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dada wa Rais Magufuli azikwa Chato

Spread the love

MWILI wa Monica Magufuli, dada wa Rais John Magufuli umezikwa leo tarehe 21 Agosti mwaka huu, nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kabla ya mwili huo kuzikwa, ilitangulia misa takatifu ya kumuombea marehemu Monica iliyoongozwa na Baba Askofu Mkuu Mwandamizi, Yuda Thaddeus Ruwaichi.

Baada ya misa hiyo, Rais Magufuli aliwaongoza mamia ya watu waliojitokeza kumzika marehemu dada yake Monica aliyefariki dunia tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa napatwa matibabu.

Viongozi mbalimbali wa serikali na wastaafu washiriki mazishi ya marehemu Monica, wakiwemo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Raila Odinga.

error: Content is protected !!