May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chama arejea, Manula, Lwanga ‘Out’ dhidi ya Mbeya City

Spread the love

Mara baada ya kukosekana Uwanjani kwa wiki tatu, kiungo wa klabu ya Simba, Clatous Chama amerejea Uwanjani, huku mlinda mlango wa klabu hiyo Aishi Manula pamoja na Thadeo Lwanga wataukosa mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City kwa kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Chama amerejea mara baada ya kufiwa na mke wake Mercy Manuka tarehe 29 Mei 2021, Kitwe nchini Zambia.

Mchezo huh, utapigwa hii leo majira ya saa 1 usiku, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Akithitisha taarifa za wachezaji hao, kocha msaidizi wa klabu ya Simba Seleman Matola amesema kuwa kiungo huyo ameshawasili kambini na kujiunga na wenzake, mara baada ya timu hiyo kurejea kutoka Mwanza.

“Kikosi kiliingia kambini jana baada ya kurejea kutoka Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa kesho na tunafurahi kiungo Clatous Chama amewasili na amejiunga na wenzake.” Alisema Matola

Aidha Matola pia alithibitisha kukosekana kwa wachezaji wawili kwenye mchezo wa leo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano, huku mmoja akiwa anaumwa.

Thadeo Lwanga, kiungo wa Simba

“Manula na Taddeo wao watakosekana kwenye mchezo wa kesho sababu wana kadi tatu za njano wakati Ibrahim Ajibu ni mgonjwa anasumbuliwa na malaria lakini wachezaji wengine wote wako fiti tayari kwa mechi,” amesema Matola.

error: Content is protected !!