Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Spika Ndugai afura bungeni
Tangulizi

Spika Ndugai afura bungeni

Job Ndugai Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania
Spread the love

 

KUKITHIRI kwa malalamiko yanaelekezwa kwa Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), yamemchefua Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaandika Yusuph Katimba…(endelea).

Kiongozi huyo wa Bunge, ameona mawaziri wanaosimamia Wizara ya Maliasili na Utalii kwamba, yanaweza kuwakuta kama yaliyowakuta watangulizi wao.

Hatua hiyo inatokana majibu ya Mary Francis Masanja, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akitoa ufafanuzi leo Jumanne, tarehe 22 Juni 2021, bungeni jijini Dodoma, kuhusu tuhuma zilizotolewa na Cecilia Paresso, mbunge wa viti maalumu asiye na chama kwamba askari wa hifadhi wamekuwa wakisababisha mauaji kwa wananchi pamoja na mifugo yao pale wanapowakuta kwenye hifadhi.

Malalamiko hayo yalikuja kupigiliwa mwongozo ulioombwa na Esther Matiko, mbunge asiye na chama wa spika kwa kutumia kanuni namba 76, baada ya kutorodhika na majibu ya naibu waziri Masanja.

Akijibu tuhuma kuhusu askari kushambulia wananchi na mifugo yao wanapokutana hifadhini, Waziri Masanya amesema, askari wa hifadhi pia wanauawa.

“Askari wetu ni wengi sana wanauawa na tulikuwa tukishambulia zaidi askari, lakini matukio yanatokea pande zote mbili kwamba askari wanakuwa kwenye sheria na kukabiliana kwenye maeneo yao ya hifadhi kwa maana ya kuyalinda hayo maeneo.”

“Inapotokea kwa wananchi kutotii sheria, basi huu mtafaruku unatokea. Lakini katika hili analoongelea kwamba waliingia na kuchoma moto, mheshimiwa spika mimi hilo siwezi kuliongelea hapa kwa sababu taarifa zake tuliishawahi kuzingongelea hapa, kwamba zipo kwenye uchunguzi na DNA zimeishapelekwa kwenye maeneo yetu ya uchunguzi na taarifa hizi ni za kiusalama zaidi,” ameeleza Waziri Masanja.

Majibu hayo yalimuinua Matiko ambaye alisema, malalamiko yametanda maeneo mengi ya Tanzania na kwamba, serikali inasimama na kusema haina taaifa ya kinachoendelea, hivyo aliomba bunge kuunda kamati maalumu ili kubaini ukweli wa mambo.

Ester Matiko, Mbunge asiye na Chama

“Kumejitokeza majibu yasiyoridhisha kutoka kwa mheshimiwa naibu waziri akidai kwamba hawana evidence (ushaidi), kwa matukio ambayo yamekuwa yakiendelea ya wananchi kuuawa eidha kwenye hifadhi za misitu au mbuga zetu za Wanyama.

“Kumekuwa na matukio haya kwenye maeneo mbalimbali, na baadhi ya wabunge humu wameishawahi kutoa maelezo binafsi, na hata maswali mbalimbali yanaelezea ni jinsi gani ndugu zetu wanapotea.

“Lakini hivi juzi kwenye Wilaya ya Kaliuwa, Tabora, kuna nyumba ilichomwa na mle ndani kulikuwa na mtoto mdogo, naye akafia ndani kwasababu eti hiyo familia ipo kwenye Hifadhi ya Isawima,” amesema Matiko.

Kutokana na maelezo ya Matiko, Spika Ndugai alisimama na kuieleza Wizara ya Maliasili na Utalii kuna jambo linaloendelea ndani ya TANAPA na kwamba, mawaziri wake wachunguze.

“Waziri, naibu waziri kwa ujumla wake, hebu kaongeeni na TANAPA, walikuwepo wenzenu wengine kabla yenu, nitatoa mfano wa muheshimiwa Kagasheki, (Balozi Hamis Kagasheki, waziri wa maliasili wa zamani) na wenzake.

“Ilikuwa hivi hivi inasemwa, watu wanauawa wanabisha, watu wanauawa wanakanusha. Tukaunda tume hapa na wakina muheshimiwa Lembeli (James Lembeli), ikaenda ikafanya utafiti, ilileta mambo ya ajabu kabisa,” amesema Spika Ndugai.

Spika Ndugai amewaonya viongozi wa wizara hiyo kutoingia kwenye mkumbo hu kwa kujaribu kuwalinda watu ambao hawalindiki.

“Mkazungumze na TANAPA, TANAPA hiyo sio hii ya sasa hivi, kuna nini? There is problem some ware (kuna tataizo mahali), mzungumze nao. Wamegeuka sasa kuwa wao ndio majangili. Ukiona wanasemwa semwa vibaya mahali fulani kila wakati, kutakuwa na shida flani.

“Na hawa wananchi wakijua, nikikutwa humu nauawa, maana yake ni kwamba mwananchi yeyote aliyeingia humu kwa sababu yoyote ile, sasa na yeye ni vita na askari na askari ni vita na wao. Tunakuwa na nchi tunasema kuna amani, kumbe kuna maeneo fulani kuna vita ndani yake,” amesema.

Spika Ndugai amehoji, kwanini tuhum za mauaji ya wananchi na mifugo yao zimeongezeka katika kipindi hiki, amemtaka waziri wa maliasili kutafuta kiini cha malalamiko hayo.

“Kwa hiyo tuangalie TANAPA, wajue hawa ni watu tu, raia wa kawaida hawa. Mbona wameishi nao huko nyuma miaka yote vizuri? Kwanini sasa hivi hali ni hii?

“Nenda kakae na watu wako, wasikudanganye, wasikupe ripoti za juu juu tu. Tazama tu kuna shida mahali, askari wengi ni vijana wameajiriwa miaka ya hivi karibuni, huenda wanafurahia tu kuuu… kuu…,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!