Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yapuliza kipyenga cha Urais
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yapuliza kipyenga cha Urais

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia ya Maendeleo (Chadema) kimefungua milango kwa watia nia wa urais wa chama hicho kuanzia leo Jumatano tarehe 3, Juni hadi Juni 15,2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu wa Chadema, Katibu Mkuu chama hicho, John Mnyika amesema watia nia hao wataandika barua kwa katibu mkuu.

Amesema, baada ya hapo, atafikisha majina ya waliojitokeza kwa kamati kuu ambayo itayapitia,”tutatoa taarifa tena ya nini kitaendelea baada ya tarehe 15 Juni 2020.”

Pia, Mnyika amesema, chama hiko kimefungua milango ya majadiliano na vyama vingine vya siasa,”vyenye dhamira ya kuiondoa CCM madarakani, tutashirikiana nao.”

Kuhusu waliotia nia mapema kama alivyofanya Dk Myrose Majige ya kutangaza, amesema,”ili utie nia, lazima uandike barua kwa katibu mkuu, lakini kama umetia nia huko kwenye vyombo vya habari, mimi siwezi kuwazungumzia.

Mnyika amewataka watia nia wote kuhakikisha wanasoma vyema mwongozo wa chama hicho wa mwaka 2012 unaodhibiti rushwa ndani ya chama.

“Wagombea wanaotarajia kutia nia, wazingatie mwongozo na kama hawatofuata, chama hakitasita kuwachukulia hatua,” amesema Mnyika

Kuhusu ubunge, uwakilishi na udiwani, Mnyika amesema, utaratibu utatangazwa baadaye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!