
John Bocco mshambuliaji wa Simba
Mshambuliaji wa klabu ya Simba John Bocco ameshinda tuzo ya kuwa mchezaji bora wa mashabiki mwezi Mei, mara baada ya kuwabwaga Thadeo Lwanga na Bernad Morrison waliokuwa wote kwenye kinyang’anyiro. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Katika michezo aliyocheza mwezi Mei katika mashindano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mshambuliaji huyo amepachika jumla ya mabao 5.
Mara baada ya kuchaguliwa kushinda tuzo hiyo Bocco atapata kitita cha shilingi 1,000,000 kutoka kwa wadhamini wa tuzo hiyo kampuni ya Emirates Aluminium.
Katika kura zilizopigwa mshambuliaji huyo ameshinda kwa asilimia 59.3, nafasi ya pili ikishikwa na Morrison aliyepata asilimia 29.4 na Lwanga alipata asilimia 11.3.
More Stories
Ni Profesa Hoseah tena TLS
Askofu Gwajima: Viongozi wa Serikali wanamchonganisha Rais
Naibu Spika awapongeza wabunge Mwambe, Rose kuoana, awapa darasa