Mara baada ya Afisa habari wa klabu ya Yanga Hassan bumbuli kusema hautambui mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa tarehe 3 Julai, 2021, kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Haji Mfikirwa amesema kauli hiyo sio ya klabu bali aliongea kama shabiki. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Mchezo huo ambapo hapo awali ulipangwa kuchezwa tarehe 8 Mei 2021 uliahirishwa mara baada ya klabu ya Yanga kugomea mabadiliko ya muda yaliofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutaka mchezo huo kupigwa majira ya saa 1 usiku na sio saa 11 katika muda wa awali.
Katika mahijiano yake siku ya jana Bumbuli alisema kuwa michezo wanayoitambua iliyosalia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ni mine ambayo ni dhidi ya Ruvu Shooting, Dodoma Jiji FC, Mwadui FC na Ihefu huku akisema mchezo dhidi ya Simba walishaucheza toka tarehe 8 Mei.
“Yanga tuna mechi nne za Ligi Kuu ambazo zimesalia, tuna mechi dhidi ya Ruvu Shooting, Mwadui FC, Ihefu FC na Dodoma Jiji FC, kuhusu mechi yetu dhidi ya Simba SC hiyo tayari tumeshacheza tarehe 08.05.2021.” Alisema Bumbuli

Mara baada ya kauli hiyo kuzua mjadala mzito kamimu katibu mkuu wa klabu hiyo Haji Mfikirwa alijitokeza hadharani na kusema kuwa kauli aliyotoa kiongozi huyo sio tamko la klabu bali alizungumza kama shabiki.
“Kauli aliyotoa afisa habari Hassan Bumbuli kutoutambua mchezo wa July 03 dhidi ya Simba SC siyo Kauli ya Klabu, bali aliongea Kama shabiki. Sisi Kama Klabu tutatoa Kauli rasmi hivi karibuni kuhusu mchezo huo.”Alisema Mfikirwa
Leave a comment