KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Etiene Ndayilagije amemuweka nje ya kikosi mshambuliaji wa klabu ya Simba John Bocco kutokana na kusumbuliwa na majeruhi na hivyo kumpa muda kwa ajili ya matibabu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Mazoezi hayo ambayo yameendelea leo kwenye viwanja vya Gymkhana Jijini Dar es Salaam kwa siku ya pili toka kikosi hicho kilivyoingia kambini siku ya Jumatatu.
Kabla ya mazoezi hayo Ndayilagije alielezea hali ya kikosi chake baada ya mazoezi ya siku mbili, huku akitoa sababu ya nahodha wa klabu ya Simba, John Bocco kutokuwepo kwenye kikosi hiko.
“Tatizo kidogo lilitokea kwa Bocco ambaye hakuwa vizuri tumeona aendelee na matibabu kwa kuwa tumeona hawezi kuendelea, lakini wachezaji wote wamefika kasoro Himidi Mao ambaye ataingia baadae lakini wote wana hali nzuri,” alisema kocha huyo.

Stars inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi siku ya Jumapili 11 Oktoba, 2020 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa majira ya saa 10 jioni katika kujiweka sawa na mchezo wa kufuzu Afcon dhidi ya Tunisia.
Leave a comment