Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 985 zitakavyoboresha elimu ya juu Tanzania
Habari Mchanganyiko

Bilioni 985 zitakavyoboresha elimu ya juu Tanzania

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania, kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , imesema itatumia mkopo wa dola milioni 425 (zaidi ya Sh.985.49 bilioni), kufanya mageuzi na maboresho makubwa ya elimu ya juu ili kukuza uchumi kwa kuwa na wahitimu wanaoweza kuajirika na kujiajiri. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano tarehe 13 Januari 2021 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kikao kazi cha wadau cha kujadili rasimu ya miongozo  ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboreshaelimu ya juu  na mabadiliko ya kiuchumi (HEET).

Dk. Akwilapo amesema, fedha hizo ambazo ni Mkopo  kutoka Benki ya Dunia (WB) ulioidhinishwa katika mkutano wa tarehe 15 Desemba 2020, utajibu baadhi ya changamoto zilizopo katika vyuo vikuu

“Mradi unakuja kujibu baadhi ya changamoto, tunazokabiliana nazo katika vyuo vikuu nchini,” amesema Dk. Akwilapo.

Katibu Mkuu huyo amesema, miongoni mwa mambo yatakayotekelezwa katika mradi huo ni kuboresha na kujenga miondombinu mingine ya kufundishia na kujifunzia, kununua vifaa, kuhuisha mitalaa “ili kuwawezesha wahitimu kuajiliwa au kujiajili wao wenyewe.”

Amesema, mradi huo pia, utawezesha kuongeza udahili wa wanafunzi vyuoni kutoka ndani na nje ya nchi  huku akikumbushia kuwa zamani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kilikuwa kikidahili wanafunzi wengi kutoka nje.”

Dk. Akwilapo amesema, kupitia mradi huo pia, wataalamu 639 watapata mafunzo na kutakuwa na mafunzo kazini ambapo vyuo 14 za umma vitahusika katika mradi huo.

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa James Mdoe alisema, lengo la kukutanisha wadau ni kupata uelewa wa pamoja ili kushauri na kuboresha kuhusu mradi huo.

Profesa Mdoe alisema, mradi wowote unahitaji kuwa na rasilimali fedha na rasimali watu na ndiyo maana walianza kutafuta fedha kuanzia Januari 2018 na kufanikiwa kuidhinishiwa mkopo huo ambao ukianza kutekelezwa, utakuwa na matunda chanya kwa nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!