MTANDAO wa kijamii wa Facebook umefungia akaundi zinazoshabikia Chama Tawala cha Uganda, NRM kinachoongozwa na rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).
Kutokana na hatua hiyo, Rais Museveni na serikali yake wameamua kufungia mitandao yote ya kijamii kuanzia jana tarehe 13 Januari, 2021.
Leo tarehe 14 Januari 2021, Raia wa Uganda wapo kwenye foleni ya kura kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Rais Musemeni amenukuliwa akisema, uamuzi huo unatokana na hatua ya Facebookkufungia akaunti za wafuasi wake.

Kwenye uchaguzi huo uliotanguliwa na mauaji ya hovyo yaliyofanywa na vikosi vya usalama kwa raia wa nchi hiyo, Rais Museveni anakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) (38), wanamuziki wa kizazi kipya.
Bobi Wine anatamba kumng’oa Rais Museveni kwa madai ya kuongoza kizazi kipya cha wapiga kura ambao ni wengi nchini Uganda, naye Rais Museveni anayegombea kwa mara ya sita akiwa madarakani kwa miaka 35 sasa, anatamba kustawisha jamii ya Waganda.
Katika kukabiliana na kile kinachoitwa vurugu, Polisi Uganda wameeleza kwamba, maofisa wake watakaa kwenye majengo marefu Kampala, ili kufautilia kila kinachotokea huku wengine wakizunguka mitaani.
Taifa hilo linaingia kwenye uchaguzi ikiwa tayari watu zaidi ya 50 wamepoteza maisha tangu kuanza kwa hekaheka za uchaguzi mkuu nchini humo.
Leave a comment