Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Baba mkwe amtaka Waziri asitumie jina la Gwajima
Habari MchanganyikoTangulizi

Baba mkwe amtaka Waziri asitumie jina la Gwajima

Spread the love

MZEE Mathias Gwajima, Baba mkwe wa Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima, amemtaka mkamwana wake huyo aache kutumia jina lake la ukoo kwa madai kwamba anaiharibu familia yake baada ya kuagiza vyombo vya dola vimkamate shemeji yake, Askofu Josephata Gwajima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ombi hilo imetolewa na Mzee Gwajima, leo Jumapili, tarehe 22 Agosti 2021, akiongea mbele ya Askofu Gwajima, katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, siku chache baada ya Dk. Gwajima kuviagiza vyombo vya dola vimhoji shemeji yake, ili athibitishe madai yake dhidi ya chanjo ya ugonjwa wa Korona (UVIKO-19).

Akizungumza kanisani hapo, Mzee Gwjaima amemuomba Dk. Gwajima ambaye ameolewa na mdogo wake Askofu Gwajima atumie jina lingine.

“Mimi namuomba bwana mdogo achukue njia nyingine, jina la Gwajima alifute kabisa. Achukue jina lingine, mimi sielewi sasa anafikiri kitu gani, yeye kama anajifanya kwamba ana akili ya kutosha basi ajitenge na mimi,” amesema Mzee Gwajima.

Mzee Gwajima ameongeza “Mimi kwa kweli usemi sina isipokuwa sasa huyu mama yetu huyu anajiita Gwajima, nasikitika sana na mimi ningekuomba hata jina la Gwajima asingelitumia, anataka kuniharibia familia yangu.”

Mzee Gwajima ametoa msimamo huo, baada ya Askofu Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumuomba ridhaa baba yake akimtaka amruhusu ampasue pasue waziri huyo wa afya, kufuatia agizo lake la kutaka akamatwe.

“Sasa nataka nimpasue pasue vipande vipande, ila sasa kwa sababu ni mkweo sitaki wewe ukasirike. Sasa mzee unasemaje?” amesema Askofu Gwajima.

1 Comment

  • Mmmmh!

    Mambo haya ni kazi sana. Kutoka uwajibikaji hadi kwenye familia.

    Mambo ya korona hadi kukamatwa. Yote kwa yote kila jambo lina mwisho wake.

    Kila aliyeumia kwenye jambo hili maumivu yake yatapita.

    Hisia zetu wanadamu ni kama mawimbi ya bahari kuna wakati yanakuwa makali na ya kutisha kuna wakati yanakuwa vivutio kwa watu.

    Hisia zina mzunguko, leo una huzuni kesho haieleweki kuwa huzuni itaondoka au la.

    Lakini mara zote hisia huwa na mzunguko. Leo utakuwa na furaha kesho inaweza kuwa tofauti.

    Rafiki yako,

    Aliko Musa.

    Mbobezi Kwenye Majengo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!