May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mahubiri ya polepole yaivuruga CCM

Humphrey Polepole, Mbunge wa kuteuliwa na aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Spread the love

 

Mbunge wa kuteuliwa na kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewavuruga makada wenzie wa chama hicho baada ya kuandika waraka mfupi huku akiwasihi Watanzania kuwa wasiogope bali wazingatie lishe bora. Anaripoti Mwandishi wetu. Endelea…

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Polepole ambaye alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi – CCM katika Serikali ya awamu ya Tano, kwenye ujumbe huo alinukuu vifungu vingi vya Kitabu kitakatifu cha Biblia na kujinasibu kuwa ujanja wake wote ni Mungu.

“Msiogope wala msifadhaike, kuhusu hili jambo tutavuka tu kubwa tuendelee kusimama katika Imani katika dini zote Mungu wa kweli muumba wa mbingu na dunia ni Mmoja. Zingatia lishe bora, shughulisha mwili wako kwa kuchapa kazi na kwa mazoezi na zile mbinu zetu, haki, hiyo kitu utaisikia tu!

“Mnapokwenda katika Ibada leo niwaache na maneno mawili Yeremia 33:3 na Mathayo 6:33. Mungu akawabariki na kuwaongeza.

Kufuatia waraka huo, kada mwenzie na mchambuzi mahiri wa siasa nchini, Thadeo Ole Mushi, alimjibu na kumpasukia hivi; “Kipindi cha JPM ulimsahau Mungu? Tulitarajia katika mambo makubwa ya kidhalimu yaliyokuwa yakitokea useme maneno haya Kwa watanzania.

“Tulitamani wakati familia ya Azory ilipokuwa ikimtafuta baba yao, wazazi wa Ben Saanane walipokuwa wakimtafuta mtoto wewe kama Mwenezi wa chama wa kipindi kile ufike kwenye hizi familia na kuwahubiria haya.

“Mungu huwa hadhihakiwi, Kwa nafasi uliyokuwepo utalipwa sawasawa na matendo yako. Wanaomheshimu Mungu na Kumwogopa hawana haja ya kutangaza mitandaoni bali matendo yao utayaona tu.”

Licha ya kwamba baadhi ya wachangiaji katika waraka huo, walimuunga mkono, mmoja wao alimuuliza kuwa baada ya kutoka mamlakani ndiyo umejua hilo, kisha Polepole akajibu hajatoka mamlakani.

error: Content is protected !!