June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kaka’ke rais aliyetimuliwa madaraka aikubali Taliban

Spread the love

KATIKA hali ya kushangaza, Kaka yake Rais aliyetimuliwa madarakani na kundi la wanamgambo wa Taliban huko nchini Afghanistan, Ashraf Ghani, Hashmat Ghani amesema anaunga mkono kundi hilo kuchukua madarakani. Imeandaliwa na Gabriel Mushi.

Aidha, amesema suala la msingi ni kundi hilo kuhakikisha linaunda serikali shirikishi.

Akizungumza na Aljazeera kusini mwa jiji la Kabul nchini humo, Ghani alisema amekuwa akionana na viongozi wa kundi hilo kwa siku kadhaa tangu Rais ambaye ni mdogo wake kuikimbia Ikulu na kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu.

Amesema kwa mazingira yaliyokuwepo pindi Marekani ilipotangaza kuondoa majeshi yake nchini humo, ni dhahiri kuwa iwapo Rais angeweka msimamo kutaka kupambana na Taliban hali ingekuwa mbaya zaidi.

Hashmat ambaye ana umri wa miaka 60 huku Rais Ashraf akiwa na miaka 79, ni mfanyabiashara mkubwa huko Kabul ambaye pia anahusishwa kuwa mshirika wa karibu wa Taliban kwani tangu kikundi hicho kiondolewe madarakani mwaka 2001 hakijawahi kuonesha kuwa tofauti naye.

Imeelezwa kuwa hata kipindi ambacho Taliban ilishika madaraka mwaka 1996 hadi 2001, haikuwahi kumzuia Ghani kuangalia televisheni licha ya kuamuru watu wote kutokuwa na tv majumbani mwao.

Pia kikundi hicho hakikumzuia kubandika picha zake kwenye kuta za nyumba yake kama ilivyokuwa kwa raia wengine wa nchi hiyo.

Taliban iliiteka Ikulu ya Kabul tarehe 15, Agosti mwaka huu na kuhitimisha safari ya miaka 20 ya utawala wa kidemokrasia nchini humo.

error: Content is protected !!