Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Baada ya kuiadhibu Real Madrid, Tuchel awamwagia sifa wachezaji wake
Michezo

Baada ya kuiadhibu Real Madrid, Tuchel awamwagia sifa wachezaji wake

Spread the love

 

BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid, kocha wa kikosi cha Chelsea, Thomas Tuchel ametoa pongezi kwa wachezaji wake kwa kufanikisha timu hiyo kufuzu kwenye fainali ya Ligi ya  Mabingwa Ulaya kwa kuwa ulikuwa mchezo mgumu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa nusu fainali ulichezwa jana kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, ambapo Chelsea ilifanikiwa kuungana na Manchester City kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa jijini Instabul nchini Uturuki tarehe 28 Mei, 2021.

Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Chelsea, Tuchel alisema walistahili kushinda licha ya kuwa mchezo mgumu kwa kuwa Madrid, walimiliki mpira kwa asilimia kubwa ila wao walikuwa bora kwenye mashambulizi ya kushtukiza (counter attack).

“Ulikuwa mchezo mgumu kwa sababu Real Madrid, walikuwa na umiliki mzuri wa mpira na walitufanya sisi kuangaika zaidi, lakini baadae tulikuwa hatari sana kwenye mashulizi ya kushtukiza na hatukupoteza hali yetu ya kuzuia,” alisema Tuchel na kuongeza;

“Kipindi cha pili tulikuwa bora sana, kwa mfumo wa kuzuia na tungeweza kupata bao la mapema sana na tungeweza kufunga zaidi, ni mafanikio makubwa na hongera kwa timu.”

Mabao ya jana ya Chelsea yalifungwa na Timo Werner kwenye dakika ya 28, na bao la pili likiwekwa kambani na Mason Mount kwenye dakika ya 85.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!