May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge Tanzania laweka historia mpya

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania

Spread the love

 

KWA mara ya kwanza, kipindi cha maswali kwa waziri mkuu bungeni nchini Tanzania, kimekosa maswali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika leo Alhamisi, tarehe 6 Mei 2021, amewaeleza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, “hakuna mbunge aliyejiandikisha kwa ajili ya kumuuliza maswali waziri mkuu.”

Hata hivyo, wakati Dk. Tulia akitoa kauli hiyo, kiti cha Waziri Mkuu – Kassim Majaliwa, bungeni kilikuwa wazi – hakuwepo hadi kipindi cha maswali na majibu kilipomalizika.

         Soma zaidi:-

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana Jumatano, tarehe 4 Mei 2021, alikuwa katika Jimbo la Buhigwe, mkoani Kigoma, akimpigia kampeni Eladory Kavejula, anayegombea ubunge wa jimbo hilo kupigia chama hicho.

Tangua kuanzishwa kipindi cha maswali kwa waziri mkuu mwaka 2007 bungeni, wakati wa aliyekuwa spika wa bunge hilo Hayati Samweli Sitta, kindi hicho hakijawahi kukosa maswali kwa waziri mkuu, ikiwa waziri mkuu siku hiyo, anakuwapo bungeni.

Kassim Majaliwa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM alipokuwa akizungumza na wakazi wa jimbo la Muhambwe

Maswali kwa waziri mkuu, huwa hayapo Alhamisi, ikiwa waziri mkuu hayupo bungeni. Ni Tofauti na leo Alhamisi, ambapo Dk. Tulia amesema, hakuna mbunge yoyote aliyejitokeza kuuliza.

Maswali hayo kwa waziri mkuu, yanasimamiwa na kifungu cha 44 (1-7), cha Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Juni 2020.

Vifungu hivyo, vinaeleza;

(1) Waziri Mkuu anaweza kuulizwa maswali na Mbunge yeyote ambayo yatazingatia masharti kuhusu maswali ya Bunge pamoja na Mwongozo uliowekwa na Nyongeza ya Sita ya Kanuni hizi.

(2) Maswali atakayoulizwa Waziri Mkuu hayatakuwa na taarifa ya awali kama maswali mengine.

(3) Kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kitakuwa kila siku ya Alhamisi na hakitazidi dakika thelathini

(4) Waziri Mkuu anaweza kutumia Kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kutoa taarifa au ufafanuzi kuhusu suala lolote linalohusiana na shughuli za Serikali na lenye maslahi kwa umma kwa muda usiozidi dakika kumi, ikifuatiwa na maswali ya Wabunge kwa dakika ishirini kuhusu taarifa yake au masuala mengine yoyote ya Serikali.

(5) Iwapo siku hiyo, kwa sababu maalum, Waziri Mkuu hatakuwepo Bungeni hakutakuwa na maswali kwa Waziri Mkuu.

(6) Pamoja na kutawaliwa na masharti kuhusu maswali ya Bunge yaliyowekwa na Kanuni hizi, maswali kwa Waziri Mkuu yatatawaliwa pia na Mwongozo uliowekwa na Nyongeza ya Sita ya Kanuni hizi.

(7) Maswali kwa Waziri Mkuu yatafuatiwa na maswali mengine kwa Mawaziri kwa dakika sitini wakati wa Vikao vya Kawaida vya Bunge na kwa dakika thelathini wakati wa Mkutano wa Bunge la Bajeti, kama yatakavyokuwa yamepangwa kwenye Orodha ya Shughuli ya siku hiyo.

error: Content is protected !!