May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam wamkabidhi rungu rasmi Moallin

Spread the love

 

KLABU ya Azam Fc inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara imemtangaza Abdihamid Moallin kuwa kocha mkuu wa kikosi hiko kwa mkataba wa miaka mitatu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Moallin alisaini mkataba huo hii leo jijini Dar es Salaam, tarehe 25 Januari 2022, mbele ya mtendaji Mkuu wa timu hiyo Abdukarim Amin (Popat).

Kocha huyo ambaye hapo awali, alirithi mikoba ya George Lwandamina, aliyetimuliwa kwenye klabu hiyo kufuatia matoke mabovu.

Mara baada ya kusaini mkataba huo, Moallin alisema kuwa anaamini uwezo wa klabu ya Azam Fc, na anaimani itafika mbali, kutokana na ukubwa walionao.

“Azam FC ni klabu kubwa, na nililiona hili siku ya kwanza tu nilipofika hapa, nina amini katika klabu hii, nina amini katika uwezo wa klabu hii, klabu hii ina nafasi ya kufanya makubwa,”- Abdihamid Moallin, Kocha Mkuu Azam FC

Kocha huyo hapo awali alikuja ndani ya Azam Fc, kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi wa Maendeleo ya Soka la Vijana, lakini alijikuta kwenye majukumu ya ukocha wa timu ya wakubwa kwa muda na kufanya vizuri kwenye michezo yake.

Toka alikabidhiwa kikosi hiko mwishoni mwa mwaka jana, Moallin alionesha uwezo mkubwa kwa kuleta mabadiliko kwenye kikosi cha klabu hiyo, huku akifika Fainali ya Kombe la Mapinduzi, na kupoteza dhidi ya Simba SC.

Katika michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara kocha huyo amepoteza mchezo mmoja tu, dhidi ya Simba kwa mabao 2-1, uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!