
LUTENI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Dennis Urio (42), amepanda kizimbani kutoa ushahidi wake, katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Urio ni shahidi wa 12 wa Jamhuri katika kesi hiyo inayosikilizwa Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.
Ofisa huyo wa JWTZ amepanda kizimbani asubuhi ya leo Jumatano, tarehe 26 Januari 2022 kutoa ushahidi wake, akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Abdallah Chavula.
Urio amesema, anatokea Kikosi 92 KJ cha Ngerengere, Morogoro cha makomandoo ambapo amedai amelitumikia jeshi kwa miaka 18.
Mbali na Mbowe, wengine ni Adam Kasemwa, Halfan Bwire na Mohamed Ling’wenya waliokuwa makomandoo wa JWTZ kikosi cha 92 KJ.
Kwa mujibu wa kesi hiyo iliyopo mahakamani hapo, Urio ndiyo anayedaiwa kumtafutia Mbowe makomandoo hao wa JWTZ.
Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali
More Stories
Msukuma: Mbowe alipa-miss Ikulu
Wabunge upinzani, CCM waungana kumpongeza Rais Samia
Dk. Mollel naye aagizwa kujibu maswali kwa ukamilifu