Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu awataka vijana kufanya kazi, kuacha utegemezi
Habari Mchanganyiko

Askofu awataka vijana kufanya kazi, kuacha utegemezi

Spread the love

ASKOFU mkuu wa kanisa la The Potter’s House Tanzania (PHCT), Ruth Kusenah amewataka vijana  wote nchini kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujiongezea kipato wao wenyewe na taifa kwa ujumla. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).

Ametoa rai hiyo leo tarehe 12 Machi 2023  katika ibada maalumu ya kutambulisha hati ya usajili wa kudumu wa kanisa hilo lenye makao yake makuu jijini Dodoma katika kata ya Ipagara mtaa wa Mlimwa west.

Amesema kuwa kanisa hilo pamoja na kuwa linawalea watu kiroho lakini bado linasisitiza waumini wake na jamii kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujipatia kipato pamoja na kulifanya taifa kuepukana na vijana wengi ambao ni tegemezi.

“Kwa sasa kanisa letu limepata usajili wa kudumu tunawashukuru sana viongozi wa serikali kwa kuweza kutambua umuhimu wa uhuru wa kuabudu, kanisa linaendelea kutoa huduma ya kiroho lakini pia tunasisitiza katika utendaji wa kazi kwa bidii kwa kazi ni mpango wa Ki-mungu pia.

“Mandiko Matakatifu yanaelekeza zaidi kuwa asiyefanya kazi na asile, lakini pia yanaelekeza kuwa Mungu atabariki kazi za mikono yetu na atabariki mashambani na mjini na aingiapo shambani na atokapo hivyo kufanya kazi ni mpango wa Mungu mwenyewe” amesisitiza Askofu Mkuu Ruthi.

Sambamba na hilo Askofu huyo amesema kanisa litashirikiana na serikali katika kufanya kazi ya kimaendeleo pamoja na kusikiliza mipango iliyo mema kwa taifa na watu wake.

Naye katibu mkuu wa kanisa hilo, Festo Lesirwa, amesema kanisa litafanya kazi na serikali kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na kuishauri serikali, kuipongeza na kuionya pale inapokuwa imeenda kinyume lakini kwa kutumia lugha za staha.

Aidha, amesema kuwa kanisa litahakikisha linalinda amani ya nchi kwa kujenga misingi ya mshikamano upendo na umoja ili kila mmoja aweze kufanya kazi kwa amani na utulivu bila kuwepo kwa migongano ya aina yoyote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!