Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya
Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the love

WAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro, uongozi wa klabu hiyo umesema ni jambo zuri kuwa na Rais wa nchi anayependa michezo kiasi cha kuongeza motisha katika utafutaji magoli muhimu ya kuzivusha timu za nchi yake kwenye michuano ya Kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yamekuja kutokana na ofa ya Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kutoa Sh milioni tano kila goli litakalopatikana kwa timu za Simba na Yanga, Simba ikishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati mtani wao wa jadi Yanga, akicheza Kombe la Shirikisho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Machi 2023, Msemaji wa Simba, Ahmed Ally amesema si tu Rais Samia anatamani timu za Tanzania zifanye vizuri Kimataifa, bali pia anashiriki kikamilifu katika mbinu ya utafutaji wa magoli muhimu ya kuzisaidia timu za nchi yake.

Amesema hali hii inaongeza chachu ya wachezaji, mashabiki, wanachama na viongozi wote kuona wana deni kubwa kwa rais wao, hivyo kuongeza bidi kubwa kushinda kwenye mechi zao.

“Si tu Rais Samia anataka twende mbele, bali pia anaingia kwenye watafutaji wa magoli, kwa maana kununua goli katika mechi ngumu kama hizi, anamaanisha anataka wachezaji wacheze jihadi ili kuyapata kwa lengo moja tu timu ishinde na kupata pointi muhimu.

“Mambo kama haya kufanywa na mtu mkubwa kama Rais wa nchi yanatia moyo, ukizingatia anayefanya haya si mtu wa kawaida isipokuwa raia namba moja kwenye Taifa letu, hivyo sisi Simba tunamuahidi makubwa mama yetu kwenye mechi yetu dhidi ya Horoya Jumamosi ijayo kwa lengo moja la kufuzu robo fainali,” amesema Ally.

Katika michuano ya Kimataifa inayoshirikisha timu za Simba na Yanga, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amejitokeza kununua kila goli litakalopatikana kwa Sh Milioni 5, ambapo mpaka sasa Yanga wamevuna milioni Milioni 30 kwa kufunga bao 6, huku Simba wao wakipata Sh Milioni 10 kwa kufunga mabao 2.

1 Comment

  • Simba na Yanga za sasa siyo bora tena. Ahadi lukuki lakini hakuna matendo. Kujichimbia au kuweka kambi mahasusu kwa ajili ya mechi ni ishara tosha timu siyo bora.
    Nilitegemea Simba na Yanga zimilikiwe na wanachama. Kama MO Dewji na wale GSM wanazipenda timu hizo, basi wangeweka lebo zao mbele ya jezi na kulipia.
    Hivi sasa wao wanamiliki zaidi ya 51%.
    Ni makosa vilabu vya wanachama kupewa matajiri. Wakaanzishe vilabu vyao. Hongera sana Bakhressa na Azam FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!