Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Xi afanya mabadiliko makubwa baraza mawaziri
Kimataifa

Xi afanya mabadiliko makubwa baraza mawaziri

Rais wa China Xi Jinping
Spread the love

Baraza Kuu la Chama cha Kikomunisti cha China limeidhinisha baraza jipya la mawaziri linaoundwa na marafiki wa karibu wa Rais Xi Jinping katika uamuzi unaozidi kumpa nguvu kiongozi huyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Mkutano huo uliwateua wajumbe waliobakia wa baraza jipya la mawaziri wakati ukielekea kuhitimisha kikao chake cha wiki nzima kinachofanyika kila mwaka jijini Beijing.

Wajumbe wapatao 3,000 waliidhinisha uteuzi wa mshirika wa muda mrefu wa Xi na mkuu wa zamani wa utumishi serikalini, Ding Xuexiang, kuwa makamu wa kwanza wa waziri mkuu, baada ya Li Qianga kuteuliwa kuwa waziri mkuu mpya jana tarehe 11 Machi 11.

Mtaalamu wa uchumi, He Lifeng, aliteuliwa kuwa makamu wa waziri mkuu mwenye dhamana ya kusimamia sera za uchumi na fedha, akichukuwa nafasi ya Liu He aliyekuwa akisimamia majadiliano ya biashara kati ya nchi yake na Marekani.

Jenerali Li Shangfu, ambaye amewekewa vikwazo na Marekani, aliteuliwa kuwa waziri mpya wa ulinzi, baada ya kuongoza programu ya uendelezaji wa silaha kwenye Kamati Kuu ya Kijeshi.

Serikali ya Marekani chini ya Donald Trump ilimuwekea vikwazo Li na idara yake ya ukuzaji wa silaha mwaka 2018.

Kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Wei Fengh, Li atakuwa mwakilishi pekee wa jeshi kwenye baraza jipya la mawaziri.

Aidha, katika hatua ya kushangaza inayokusudiwa kuimarisha imani kwenye uchumi wa China, Xi aliwabakisha Liu Kun kwenye wizara ya fedha, Wang Wentao kwenye biashara na Yi Gang kuendelea na ugavana wa benki kuu.

Xi mwenye umri wa miaka 69 alikabidhiwa muhula wa tatu wa kuongoza chama na serikali tarehe 10 Machi 2023, baada ya kuondosha ukomo wa umri na mihula katika mkutano mkuu wa chama uliofanyika mwezi Oktoba, akiimarisha nguvu zake kwenye taifa  hilo la pili kwa uchumi mkubwa duniani.

Kwenye mkutano wa mwaka huu, wajumbe pia waliidhinisha mipango ya Xi kuhusu mabadiliko makubwa kwenye serikali katika miaka ya hivi karibuni. 

Mipango hiyo inajikita kwenye nafasi ya China kama kiongozi wa teknolojia na inahusisha kukata kiasi cha 5% ya nafasi za ajira serikalini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!