MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba, amesema asilimia ya 96 ya Watanzania wamefikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu. Anaripoti Jonas Mushi…(endelea).
Mashiba amebainisha hayo leo Jumatatu tarehe 13 Februari 2023 wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo katika kuhahakikisha huduma nzuri ya mawasilino nchini.
Amesema kabla ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka 2009 ni asilimia 45 tu ya Watanzania walikuwa wamefikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu kutokana na uwekezaji mwingi wa miundombinu kufanyika mjini.
Amesema idadi hiyo ya watu wanapata huduma za mawasilino ya simu kwa viwango tofauti ambapo asilimia 96 ni 2G na asilimia 72 kwa 3G na asilimia 55 wanapata 4G.
Kwa upande wa eneo la kijografia Mashiba amesema tayari asilimia 69 ya eneo la Tanzania limefikiwa na mawasiliano ya simu.
“Kijiografia hatujafanya vizuri sana na hii ni kutokana na maeneo mengi kuwa wazi na mengine kuwa ni hifadhi,” amesema Mashiba.
Leave a comment