HATIMAYE Lionel Messi wa Argentina, amenyakua taji la ubingwa wa kwanza la Copa America, akiwa na timu ya Taifa, baada ya kuifunga Brazil 1-0. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Ni baada ya kushinda katika fainali ya Copa America dhidi ya wapinzani wao wakubwa Brazil kwa bao 1-0, lililofungwa dakika ya 22 na Angel Di Maria.
Fainali hiyo imeanza kuchezwa saa 9 usiku (kwa saa za Afrika Mashariki) ya tarehe 11 Julai 2021, katika dimba la Rio wa Maracana.
Ilikuwa fainali iliyosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka kutokana na kuwakutanisha wachezaji mashuhuri duniani, Messi na Neymar Junior wa Brazil.

Wawili hao, wamewahi kucheza kwa mafanikio wakiwa Barcelona ya Hispania. Hata hivyo, Neymar alihamia PSG ya Ufaranca na Messi anaendelea kukipiga kwa miamba hiyo ya Hispania.
Argentina, imenyakua ushindi huo baada ya kusubiri kwa miaka 28, kwani mara ya mwisho ilitwaa mwaka 1993.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika, ilishuhudiwa Messi ambaye ni nahodha wa kikosi hicho, akianguka chini kwa furana na wachezaji wenzake kwenda kumbeba juu juu wakishangilia.
Wakati huo, mchezaji mwenzake, Neymar akiwa haamini kilichotokea na waliokena baadaye wakikumbatiana na wote, walivalia jezi namba 10.
Katika mchezo huo, kila mmoja alionekana kuhaha huku na huko kuhakikisha anaisaidia timu yake kunyakua ubingwa huo, lakini bahati ikawa kwa Rafiki yake, Messi kubeba ndoo hiyo.
Leave a comment