Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Tanzania yatangaza takwimu za Covid-19, “284 wanapumulia mashine”
AfyaTangulizi

Tanzania yatangaza takwimu za Covid-19, “284 wanapumulia mashine”

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imetaja takwimu za wagonjwa wa  wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19), ikisema nchi nzima ina wagonjwa 408. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Takwimu hizo zimetolewa leo Jumamosi, tarehe 10 Juali 2021 na Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima, akitoa takwimu za mwenendo wa wimbi la tatu la Covid-19, alipotembelea mnada wa Msalato jijini Dodoma.

Waziri huyo wa afya amesema, hadi kufikia tarehe 8 Julai 2021, wagonjwa 284 kati ya 408 wanapumua kwa kutumia mashine za oksijeni ‘Oxygen Concentrator”

Akitoa takwimu za jiji la Dodoma, amesema lina wagonjwa 26, kati yao 22 wanapumua kwa msaada wa mashine. Amesema hakuna kifo.

Dk. Gwajima amewataka Watanzania wazidi kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo, kwa kufuata miongozo ya wataalamu wa afya juu ya kujikinga nao.

Amewataka Watanzania wavae barakoa, waepuke mikusanyiko pamoja na kunawa mara kwa mara kwa kutumia maji tiririka.

Takwimu hizo zimetolewa takribani mwaka mmoja, tangu Tanzania kutoa takwimu za ugonjwa huo 2020.

Mara ya mwisho Tanzania ilitoa takwimu za ugonjwa huo, tarehe 28 Aprili 2020, kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliyesema kulikuwa na wagonjwa 480.

Tanzania ilitoa takwimu za Covid-19, takribani mwezi mmoja, tangu iliporipoti kisa chake cha kwanza cha ugonjwa huo, Machi 2020, baada ya hapo ilisitisha kutoa takwimu hizo kwa maelezo kwamba maabara iliyokuwa inapima wagonjwa wa Covid-19, ilipata hitirafu.

Dk. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Hatua hiyo ya Tanzania kurejea katika desturi ya  kutoa takwimu za Covid-19, ni muendelezo wa hatua zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, katika kukabiliana na janga hilo.

Tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, Rais Samia amechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuunda timu ya wataalamu, kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya mwenendo wa ugonjwa huo.

Pia, ameunda muongozo wa uingizaji na utoaji chanjo ya Covid-19, unaotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni. Kupitia mpango huo, wananchi watakaohitaji watapatiwa huduma hiyo bure.

Mara kadhaa Rais Samia amewaomba Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya Covid-19, hasa kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono na kuepuka mikusanyiko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!