Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Aliyeporwa ‘Range’ na Makonda alipuka, amtaja mtoto wa Malecela, amuangukia Samia
Habari MchanganyikoTangulizi

Aliyeporwa ‘Range’ na Makonda alipuka, amtaja mtoto wa Malecela, amuangukia Samia

Patrick Christopher Kamwelwe
Spread the love

MFANYABIASHARA Patrick Christopher Kamwelwe mkazi wa New York nchini Marekani ameshusha tuhuma nzito dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Tuhuma hizo zinahusu madai ya kumpora gari lake aina ya Ranger Rover na kuibandika namba za RC DSM (Mkuu wa mkoa Dar es Salaam) kipindi akiwa kwenye wadhifa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamwelwe ambaye pia anajulikana kwa jina maarufu kama PCK amedai Makonda anaendelea kuitumia gari hiyo hata baada ya kuondolewa madarakani licha ya kwamba si mali yake halali.

Akizungumza na Raia Mwema katika mahojiano maalum Kamwelwe ambaye ni mzaliwa wa Mpanda mkoani Katavi aliyekuwa akiishia jijini Dar es Salaam kabla ya kukimbilia Marekani kutokana na vitisho, amedai kwamba baada ya kufuatilia ili arejeshwe gari hiyo nyeusi yenye thamani ya Sh milioni 220, ndipo vitimbi na vitisho vilipoanza na kubambikiwa kesi ya jinai kwa kumiliki mali haramu.

Alidai kutokana na tuhuma hizo Juni 2017 alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku akaunti zake za benki pamoja na mali zake zikishikiliwa hadi sasa.

GARI ILIVYOKWAPULIWA

Kamwelwe ambaye awali alikuwa mfanyabiashara wa magari, msanii wa Bongofleva na promota wa muziki, alisema mwaka 2017 alifuatwa na mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, Samwel Malecela, William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz na kumueleza kuwa Makonda…. kwa taarifa zaidi soma gazeti la Raia Mwema la leo tarehe 31 Agosti, 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Total Energies yawekeza bilioni 17 kusambaza gesi ya kupikia

Spread the loveILI kurahisisha upatikanaji wa gesi ya kupikia kwa gharama nafuu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Taifa Gas waanika mikakati kupunguza gharama za gesi ya kupikia

Spread the loveKATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha...

Habari za SiasaTangulizi

Haya hapa majina walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali CHADEMA

Spread the loveCHAGUZI wa kanda za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Uingereza yamwaga bil. 9 kumuunga mkono Samia matumizi nishati

Spread the loveWaziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani...

error: Content is protected !!