Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo: Bajeti kuu haina vipaumbele vya kuboresha maisha ya Watanzania
Habari za SiasaTangulizi

ACT-Wazalendo: Bajeti kuu haina vipaumbele vya kuboresha maisha ya Watanzania

Spread the love

CHAMA Cha ACT-Wazalendo, kimekosoa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2023/24 na kudai kuwa haijaweka vipaumbele vinavyolenga kuboresha maisha ya wananchi hususan upatikanaji wa ajira. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akichangia bajeti hiyo leo tarehe 17 Juni 2023, Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Ester Thomas, amesema bajeti hiyo haijaweka mkazo katika ukuzaji sekta zinazotoa ajira kwa wananchi ili kupunguza umasikini na kuimarisha uchumi wao.

“Uchumi usiozalisha ajira sio uchumi jumuishi ni hatari, bajeti haijaoneysha mpango wa kutatua tatizo la ajira nchini hasa kwa vijana. Ukutazama sekta tano zenye uwezo wa kuzalisha ajira mfano ya nguo, haijawekewa kivutio chochote,” amesema Ester.

Ester ameshauri Serikali iboreshe bajeti hiyo kwa kuongeza fedha zitakazoimarisha sekta zinazozalisha ajira Kwa wingi ikiwemo ya kilimo na Uvuvi.

Amesema sekta zinazokuwa kwa kasi  hazitoi nafasi nyingi za ajira.

Hali kadhalika, Ester ameshauri Serikali iboreshe bajeti hiyo  kwa kuongeza fedha za kununua vyakula ili kukabiliana na mfumuko wa bei ya bidhaa hizo muhimu, hususan mchele, mahindi na maharage.

Katika hatua nyingine, Ester amesema bajeti haiajweka mfumo mzuri wa kuweka bima ya afya kwa wote kwa kutowekeza fedha kwneye mfumo utakaoimarisha afya za Watanzania.

“Serikali itapaswa kutenga fedha sawa na asilimia 2.5 ya pato la Taifa kuweza hudumia mfumo wa hifadhi ya Jamii kwa watu ambao wana fao la matibabu, kwa mfumo huu Kila mtanzania atakuwa na bima ya Afya hivyo asilimia 2.5 ya pato la Taifa iende katika hifadhi ya Jamii tunamaini bila bima afya zetu zinatetereka na kuwa na nguvu kazi ambayo haina afya Bora ya kuzalisha,” amesema Ester.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!